December 8, 2019





Na Mwandishi Wetu
MSIMU wa 2019/20 katika Bundesliga unaonekana kuwa tofauti sana na kuwashangaza mashabiki wengi hasa wanaofuatilia.


Kwa wengi wanaofuatilia kwa hapa nchini wanaangalia mechi za Bundesliga kupitia Startimes ambao wamekuwa wakirusha mechi zao moja kwa moja kwa mfumo wa High Definition au HD.


Kumekuwa na mambo mengi ambayo yanaonekana ni kama mazoea ndani ya Bundesliga. Lakini sasa mambo ni tofauti kabisa kwa kuwa kila kilichozoeleka kinakwenda kwa mwendo tofauti na uliozoeleka.


Wakati zimefika mechi 13 kwa kila timu, ilikuwa ni kawaida kabisa kuwaona Bayern Munich, Borussia Dortmund au Schalke 04, mmoja wao akiwa kileleni. Lakini sasa waliojitahidi ni Bayern walio katika nafasi ya tatu.


wanafuatiwa na vigogo wenzao, Schalke 04 katika nafasi ya nne na Dortmund wanakamilisha tano bora. Hakuna aliyeshika nafasi ya kwanza au ya pili. Wanavyokwenda, huenda wakaanza kurejea kileleni taratibu lakini kama hawapo pale hadi mechi ya 13, maana upinzani unazidi kupanda katika Bundesliga.


Kwa sasa, pia inaonekana ligi hiyo kuwa na presha kubwa zaidi hadi kwa timu vigogo tofauti na misimu minne hadi nane iliyopita kwa kuwa timu hizo kubwa nazo zimeingia katika listi ya timu ambazo zimekuwa zinajifunga au maarufu kama kujitoboa.


Timu kujifunga lazima iwe kwenye presha, kwamba wameshambuliwa sana au beki alikuwa katika presha wakati akijaribu kuokoa anajikuta akiangukia katika kujifunga.


Kwa misimu miwili hadi minne, haikuwa rahisi kuona ndani ya mechi 13 tu, tayari timu kubwa au vigogo wako kwenye listi ya timu zilizojifunga na ikiwezekana wanaongoza kwa kujifunga.


Mfano sasa, Dortmund ndiyo wanaoongoza kujifunga katika Bundesliga. Ndani ya mechi 13, tayari wamejifunga mabao matatu ambayo ni mengi zaidi kwao kwa misimu zaidi ya mitatu.


Kwa hali inavyokwenda, huenda wakaongeza kujifunga na hasa kama presha itazidi kuwa kubwa, jambo ambalo linaweza kuzua mjadala zaidi.


Timu mbili zinazofuatia kwa kujifunga zaidi ni Hertha Berlin na Augsburg. Hertha Berlin pia imekuwa si timu inayoingia katika anga hizo lakini angalau Augsburg wao wanaonekana mara kadhaa wamekuwa wakiingia.


Ndani ya listi hiyo pia unawaona vigogo wengi ambao wakati mwingine walikuwa wanamaliza msimu mzima bila ya kujitoboa hata mara moja nao wamo sasa.


Mfano Werder Bremen ambao wamejifunga mabao mawili pia lakini kuna Schalke 04 na Eintracht Frankfurt nao tayari wamejifunga bao moja kila mmoja. Hali inayoonyesha kuwa mambo bado ni magumu kwa maana ya press.


Mara nyingi, presha inazalishwa ubora wa mpinzani. Hii maana yake ubora wa timu nyingine umekuwa ukiendelea kupanda na kusababisha presha hadi kwa vigogo.


Mara nyingi timu maarufu au kubwa zimekuwa hazina presha kubwa kutokana na kiwango cha kujiamini ambacho kinatengenezwa na ubora wanaokuwa nao.


Safari hii mambo ni tofauti, hata timu nyingine nazo zinajiamini hali inayoonyesha kuwa zina ubora na sasa umepanda zaidi.


Kwa upande mwingine, pamoja na kupata shida hiyo ya kuingia kwenye presha hiyo hadi kuwa katika timu zilizojitoboa mapema kabisa. Timu vigogo zimeendelea kuwa na ubora katika ushambulizi jambo ambalo linaonyesha wana nafasi ya kurudi kileleni.


Bayern ndiyo timu inaongoza kwa kupiga mashuti mengi zaidi katika milango ya wapinzani baada ya kushindilia mikwaju 230 wakifuatiwa na Eintracht Frankfurt wenye mashuti 210 ndani ya mechi 13 na nafasi ya tatu ni Bayer Leverkusen wenye mashuti 206.


RB Leipzig wana mashuti 198 na Werder Bremen mashuti 194 na hawa wanafunga tano bora ya timu zinazopiga mashuti mengi zaidi langoni mwa wapinzani.


Kawaida kama unapiga mashuti mengi zaidi, hata kama utakosa lakini kuna nafasi ya kufunga baada ya kujirekebisha na hii ni sehemu ya kuonyesha vigogo kuna jambo wanatengeneza.

KUJIFUNGA…
1. Dortmund 3
2. Hertha Berlin   2
3. FC Augsburg   2
4. Werder Bremen  2
5. Dusseldorf 1
6. FC Koln   1
7. FSV Mainz   1
8. Hoffenheim   1
9. Schalke 04   1
10. Frankfurt 1


KUPIGA MASHUTI...
1. Bayern 230
2. Frankfurt 210
3. Leverkusen   206
4. RB Leipzig   198
5. Werder Bremen  194
6. M’gladbach 191
7. FSV Mainz    186
8. Dusseldorf  174
9. Dortmund   171
10. Hoffenheim   169



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic