DIAMOND AZIDI KUMPIGA GEPU ALIKIBA, AWAVUTA
Pasi na shaka, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ni mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki na hata barani Afrika, hivyo maisha yake yanawatamanisha vijana wengi.
Hii imedhihirishwa wazi na aina ya magari anayomi liki pamoja na makazi yake ya kifahari. Diamond au Mondi ambaye pia anapenda maisha ya kifahari, anasifika kwa kutupia mavazi ya kipekee ambayo mengi ni ya bei mbaya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye kipengele cha Insta Story (IS), Mondi alitupia video akiwa chumbani kwake ikionesha viatu vyake vingi vya bei mbaya na kuwauliza mashabiki wake ni viatu gani wangependa avae kwenye sherehe ya mwanaye, Naseeb JR iliyofanyika katikati ya wiki hii nyumbani kwa mama Mondi, Madale-Tegeta jijini Dar.
Mbali na video hiyo ya viatu vya maana kutoka kampuni zenye majina makubwa duniani, vinavyoendana na fasheni, pia alitupia video akiwa chumbani kwake akionesha Tuzo ya AFRIMA ambayo alishinda hivi karibuni.
Video hizo mbili hasa ile ya viatu ilivutia wengi huku baadhi ya watu wakimuomba japo pea moja kutokana na wingi wake kiasi ambacho mtu anaweza kufungua duka kubwa la viatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment