December 1, 2019


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kuwa kama kweli inamuhitaji mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Heritier Makambo iwe tayari kumlipa mshahara wa dola 7000 (zaidi ya Sh Mil. 17) kwa mwezi na kama akisaini mkataba wa mwaka watalazimika kumlipa Sh mil 204 kwa miezi 12.

Kauli hiyo aliitoa kocha huyo ikiwa ni saa chache mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa jijini Dar es Salaam akitokea DR Congo.

Makambo aliyeuzwa Klabu ya Horoya ya Guinea, hivi karibuni alihusishwa kurejeshwa kwa mkopo Yanga kutokana na kutopata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Zahera alisema kuwa, ni ngumu kwa Yanga kumrejesha Makambo kutokana na mshahara anaoupata ambao timu hiyo hivyo anaona  kama Wanajangwani hao hawana uwezo wa kumlipa.

Zahera alisema kuwa, hadi hivi sasa hakuna mazungumzo yaliyofanyika kati ya Yanga na Makambo, yeye bado anaendelea na majukumu yake ya kuichezea timu yake.

Aliongeza kuwa kwa hali ya kiuchumi iliyokuwepo Yanga ya kuchelewesha mishahara ngumu kwake kurejea ambayo hivi sasa inakwenda mwezi wa pili wachezaji wote hawajalipwa mishahara.

“Nikuhakikishie kuwa Makambo hawezi kuja tena kuichezea Yanga, labda baada ya hali ya kiuchumi kukaa sawa lakini siyo hivi sasa kulipa mishahara yenyewe ni shida.

“Yanga hawana uwezo wa kumlipa mshahara wa dola 7000 kwa mwezi ambao yeye anauchukua huko Horoya, kama watakuwa na uwezo wa kumlipa, basi atarudi tena.

“Kingine nikutoe hofu tu, hakuna chochote kinachoendelea kati ya Yanga na Makambo kwani hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika ya kumrejesha katika dirisha dogo la usajili,” alisema Zahera.

4 COMMENTS:

  1. Kweli ww ni wakala wake, ulivyokuwa unakataa kuwa wewe si wakala wa makambo, nina wasiwasi hata kwa molinga david falcao

    ReplyDelete
  2. Wachezaji wote wenye chembechembe za Kikongomani ndani ya Yanga wanatakiwa kuondolewa maana watakuja kujenga vimelea vya mwinyi zahera.

    ReplyDelete
  3. mmh, nilidhan uongoz haujakutendea haki, kumbe ulikuw sahihi kabsaa, bora uliondolewa maana huna jipyaa

    ReplyDelete
  4. Wakongo ndani ya yanga wataharibiwa na Zahera. Mfano Molinga kuna siku alinuna baada ya kupumzishwa na Mkwasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic