December 11, 2019


Mwenyekiti Mkuu wa klabu ya Yanga, Dr. Mshindo Msolla, amesema kuwa kamati maalum inayohusika na mchakato wa mabadiliko inaendelea vizuri.

Msolla ameeleza kuwa kwa sasa kamati hiyo inaendelea na kazi vema na kufikia mwezi Mei mwakani kila kitu kitakuwa kimekamilika.

Mwenyekiti huyo ambaye bado hajatimiza mwaka tangu achaguliwe ndani ya uongozi huo, ameeleza kwa kuwataka wanayanga wawe na subira hivi sasa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.

"Mchakato wa mabadiliko unaenda vizuri.

"Kamati ambayo ambayo inahusikana na suala hili imefikia pazuri na inaendelea na kazi.

"Tunawaahidi kufikia mwezi Mei mwakani kila kitu kitakuwa kimeenda sawa."

3 COMMENTS:

  1. Mabadiliko ya Uendeshaji na kuifanya timu kuingia kwenye uwekezaji .....NINASHANGAA M/KITI ANASEMA ILE KAMATI ILIYOUNDWA INAENDELEA NA MCHAKATO KUTOKA MWAKA JUZI IMEKUWA NA VIKAO VINGI SANA YAANI WANASEMA MPAKA MWAKANI MWEZI WA 6....SASA WATAKUWA WAMECHUKUA MWAKA. 1 1/2...HUKU MNALIA GHARAMA ZA UENDESHAJI NA MAPATO HAYALINGANI NA MATUMIZI........MNATEGEMEA KUONGEZA WANACHAMA KUANDIKISHA WANACHAMA ILI MPATE FEES ILI ZIENDESHE KLABU KUBWA KAMA YANGA??? DAWA NI KUINGIA UBIA/UWEKEZAJI NDANI YA SIKU 60 HAKUNA MUDA WA KUSUBIRI KWAKUWA MMESHAPOTEZA MUDA MWINGI KATIKA MICHAKATO....KUNA VITU VINATAKIWA MITAJI MIKUBWA YA FEDHA KAMA USAJILI, KAMBI, POSHO, UJENZI WA VIWANJA VYA MAZOEZI (KIGAMBONI & KAUNDA) AMBAPO NI MATAJIRI WENYE UWEZO WA KIFEDHA WANAWEZA KUTATUA HILI.....MSIWE NA MAWAZO YA KARNE YA 18...KUTAFUTA MICHANGO KUTOKANA NA KUINGIZA WANACHAMA WAPYA HIZO NI NDOTO HAMUWEZI KUFANIKIWA...100% WANACHAMA KULIPA MICHANGO HAWAWEZI.....KUTOKANA NA UHALISIA WA UCHUMI UNAOBADILIKA KWA KASI

    ReplyDelete
  2. Kamati hiyo kwanza ameunda lini ? Kamati nnayo ikumbuka Mimi ni ile ya mzee mgongolwa sasa kuna Nyingine tena?

    ReplyDelete
  3. Mimi ni Yanga. Huu ni muendelezo wa longolongo. Timu ina kamati 10 wenye wsjumbe 100!!Wanini wote?Nä wote wanakula.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic