December 11, 2019


Inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga uko kwenye harakati za kumalizana na straika Tariq Seif kutoka Dekernes FC ya Misri.

Mabosi wa mabingwa hao wa kihistoria kunako Ligi Kuu Bara wameanza mchakato wa kupata saini yake ikiwa zimesalia siku chache kuelekea dirisha dogo.

Kuna uwezekano Seif akamalizana na Yanga kesho kwa kutambulishwa rasmi na wakati akimalizana na wakongwe hao, Seif amefanikiwa kuingia kambani mara tano tangu asajiliwe na waarabu hao.

Mbali na kufunga mabao matano, Seif amefanikiwa kutengeneza nafasi tatu za kufunga.

21 COMMENTS:

  1. Watani acheni mbwembwe za kijinga jitahidini kwanza mumalize madeni ys wachezaji na bench la ufundi.Sijui inakuwaje hao mlio nao mnashindwa kuwalipa.Sasa mnataka kuongeza mzigo tena???

    ReplyDelete
  2. Dekernes ni timu ya daraja la pili hapa Misri. Na ni timu mbovu isiokuwa na mchezaji wa maana.Kusajili kutoka hapo ni upuuzi tu.Timu yangu sijui nani ni scout?Au ndio dili za kupiga pesa?

    ReplyDelete
  3. huyo Tariq ni Mtanzania kwaiyo hakuna shida sio foreigner

    ReplyDelete
  4. Namfahamu Tariq. Ni mchezaji wa kawaida sana na mshabiki mkubwa wa Simba. Rafiki yake ni Malika Ndeule, mchezaji wa zamani wa Azam na Mwadui. Halafu eti YANGA WAONYESHA JEURI YA PESA! Upuuzi mtupu. Watu wenye madeni mpaka kwenye kope wanawezaje kuwa na jeuri ya pesa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie Simba muwe na akili. Simba haina hela. Fedha iliyopo pale na ya urithi wa Mo kutoka kwa babake. Hebu niambieni chanzo cha mapato kimoja cha Simba. Simba bila Mo haina tofauti na Yanga. Jamani Watanzania hatujamwelewa tu Rais wetu Magufuli? Tuache kutegemea akili ya mtu au hela. Hayo majibizano ya Simba ni tajiri yananipa mashaka sana ba uwezo wetu wa akili. Tuige jeuri ya Rais wetu mpendwa Magufuli. Angalie hataki kupanda ndege eti kwenda kumpigia magoti mtu atape msaada. HAKUNA MSAADA WA BURE NDUGU ZANGU. Hizo fedha hao jamaa hawaziokoti!!!. Wakusaidie wewe mlemavu. LET US THINK OUT OF THE BOX.

      Delete
    2. Halo man city bila pesa za mwarabu ungewaona kwenye top 4 ya premier league.mpira niuwekezaji weka pesa upate pesa au wwe unadhani mo kaweka bilioni zake simba bure.niilibiashara yake iendelee kutanuka zaidi Africa nzima kupitia simba.ndo ujue kwamba hatukopeshi kaweka ili simba ikue nayeye pia akue kibiashara kuna ubaya hapo huo ndo uwekezaji kaa kwakutulia

      Delete
    3. Usihangaike kutoka nje ya box kufikiri think inside the box before hujatoka utapata majibu.unahangaika kutoka nje ya box wakati majibu yapo ndani umeyaacha.unamtolea mfano hadi rais maguful angekuwa naakili kama zako nchi ingesha toka outside the box

      Delete
    4. Daah itabidi uende darasani kidogo ndugu yangu. Concept za Out of the box zinakutoa nje. Ulianza na hoja nzuri lkn usiyoielewa kwa sababu umeambiwa tu juu ya uwekezaji bila bila kujua aina zake. Uwekezaji huu wa Simba ni kama ndoa ya mke au mme wa nyumbani. LEO UKIAMBIWA AUSSEMS KOCHA MZURI WOTE MNAUNGA MKONO KOCHA MZURI. KESHO UKIAMBIA NA MTU YULEYULE AUSSEMS KOCHA MBAYA WOTE MNAITIKIA KOCHA MBAYA. TUNAAMBIWA HAWA WABRAZIL WAZURI ETI WANAKOSA NAFASI TU NASI TUNAUNGA MKONO. Ukiona hiyo hali hapo weka mashaka makubwa. JAMANI MNATUAIBISHA HIKI SI KIZAZI CHA KIJINGA KIASI HICHO!!! AIBU!! TUFUNGUKE!! Umemsikia Aussems alichotuambia? Watu wasiofikiri wanasema eti katukana!!

      Delete
    5. Kwa hiyo tukubali Yanga wameonyesha jeuri ya pesa? Pesa ziwe za Mo, za babake au hata za mamake ndio uwekezaji huo, baada ya kuona wananchi hawachangi Profesa nae anawatafutia Mo wenu. In sha Allah mtapata.

      Delete
  5. Jamaniee mmesikia yanga wameshavunja mkataba na juma balinya yule waliye msajili kisa story za magazeti zilisema simba wanamtaka.wakamtambulisha kwa mbwembwe namajivuno ciku ya kubwa kuliko au sio yule waliyemtambulisha kwa mbwembwe zote kuwa wamemzidi kete mtani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani nyie mnatofauti gani? Hamkumbuki wale waBrazil walivyosajiriwa? On siku ile yule mBrazil alivofunga goli mechi ya kirafiki alishangilia hadi anataka kuwa kichaa. Huo ni usajili au ndo yaleyale. Miraji ni bora mara mia kuliko hao wa Brazil. Jamani unaposema nyumba ya jirani angalia kwanza ya kwako. Watanzania tuwe na critical thinking.

      Delete
  6. Sasa muandishi tushike lipi.Yanga Ina jeuri ya pesa au ina shida ya pesa?

    ReplyDelete
  7. Tofauti ys Simba na timu yetu ya Yanga ni kwamba Simba wana mipango endelevu.Wanalipa mishahara hawana longolongo za kusingizia ukata.Mwenyekiti wetu amezungumzia madeni mbona hazungumzii mapato. Timu ina wafadhili 4.Hamna mipango ya muda mrefu bora mkono uende kinywani. Tusijilinganishe na Simba wao kila siku wana improve kiuutendaji sisi tumebaki kujaribu kuangalia makosa yao madogo.Simba sasa wana viwanja sisi tuna mapori na vifusi.Tuna mfadhili GSM ambaye atakimbia kwa ubabaishaji wetu na ulaji uliokithiri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mipango ya Simba inayotegemea mtu inaweza kuwa endelevu au isiwe endelevu. Kwa mfano mimi nisingekubali kwenda Bunju kushangilia uzinduzi wa uwanja wa Simba bila kujua umejengwa kwa mapato yanayotokana na mfumo gani. Ni sawa unaletewa ule kuku nyumbani huku ukiwa na uhakika huna fedha za kula kuku. Naendaje kushangilia kitu ambacho ujenzi wake anaufahamu Mo peke yake. Si ajabu hata Asset hiyo isiwe endelevu. Mfano mdogo tu hapa nchini tuliachiwa mashirika ya Reli ya TRC na TAZARA yakiwa na kila kitu mpaka reserve ya mafuta na spares. Jiulize leo yako wapi? Hata kupaka rangi majengo wameshindwa. Jiulize majengo ya Club Msimbazi na Jangwani leo yapo ktk hali gani? Jiulize leo Mo (hatuombei) ghafla ametutoka unadhani familia yake yote inamapenzi na mpira? JAMANI LET US THINK BIG!

      Delete
  8. Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
    Unajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup


    Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji

    1. Sadney Urikhob

    2. Juma Balinya

    3. Maybin Kalengo
    Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
    Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikiwa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
    Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa

    Ahsanteni

    ReplyDelete
  9. yanga yakimataifa tunataka viwango sio mchezaji katoka team ya wapo

    ReplyDelete
  10. YANGA imefulia. Simba ina muekazaji lakini Yanga ina mzee akilimali Mungu amjaalie uzima. Simba imefika robo fainali klabu bingwa Africa ila Yanga katika jitihada za kutaka kuionesha simba kuwa wao wapo juu wakaaishia raundi ya pili. Simba ni kampuni wakati Yanga ni genge la wababaishaji. Simba inaviwanja vyake Yanga wana madimbwi ya maji. Simba wanaongoza ligi kwa point nyingi tu zidi ya Yanga.Na Wakati Simba ikifanya mikakati ya nguvu ya kuleta wachezaji wa viwango dirisha dogo utaona hata Mo yupo Uganda mara hii kule challenge cup anataka ajiridhishe kwa wachezaji wa viwango yeye mwenyewe kabla kusajiliwa lakini yanga wanasajili mchezaji kwa kusikia matandaoni. Yaani Yanga bure kabisa .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnaongoza ligi kwa kununua mechi? Mo mwenyewe ameona aibu hadi amefukuza kocha!!

      Delete
  11. Tarehe 4 pia mtasema tumenunua mechi. Wapuuzi wakubwa. Kisingizio chenu kumekuwa kujipa moyo kwenye ujinga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic