December 7, 2019


Ama kweli Yanga imepania kuwachakaza wapinzani wapo wa jadi, Simba katika mechi ya watani wa jadi inayotarajiwa kuchezwa Januari 4, kufuatia mipango waliyojiwekea ya kufanya ziara maalumu mikoani itakayoanza Desemba 10, mwaka huu.

Simba na Yanga zinatarajia kukutana Januari 4, mwakani ikiwa ni mchezo wa kwanza kukutana tangu msimu huu wa 2019/20 uanze kutimua vumbi Agosti.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa, timu hiyo inatarajiwa kuanza ziara za mikoani mara moja kabla ya kambi rasmi kwa ajili ya kuwakabili Simba.

“Tunatarajia kufanya ziara katika mikoa mbalimbali ili kuweza kuwapelekea wananchi timu yao waweze kuiona katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Kigoma na Rukwa.

“Lengo la kufanya ziara hiyo ni kuipa nafasi timu iweze kucheza mechi kadhaa za kirafiki katika kila mkoa ambapo tutapita lengo ni kuiweka timu kuwa fiti na kuwapa nafasi wananchi waione timu yao.

“Mechi ya Simba bado sana hivyo tukimaliza ziara katika mikoa hiyo ndiyo tutaangalia kambi kwa ajili ya mchezo huo,” alisema Mwakalebela.

4 COMMENTS:

  1. Yanga wawe wakweli . kuipleka timu mikoani sio kuwa ikonekane , bali ni mbinu za kujaziliza bakuli lao ili wapate vijiposho kwa wachezaji wao ili kuwamotisha kwa mechi ambayo watachezea kichapo dhidi ya mnyama tarehe 4.1.2020

    ReplyDelete
    Replies
    1. We lofa nini Kwa akili yako unadhani mikia fc mna timu ya kumfunga yanga? Yanga ni timu ya wananchi lazima wananchi waione tofauti na mikia fc ambayo ni ya Mo

      Delete
  2. Yanga bhana! Hawataki kukubali hali halisi kwamba wapo apeche alolo. Halafu mara nyingi wanapofulia, kama hivi sasa, wanapenda kujiita timu ya wananchi. Wakiwa nazo kidogo utasikia wanajiita 'Dar es Salaam Young Africans.' Hao ndio Gongowazi!

    ReplyDelete
  3. Kwamba Yanga itafungwa na Simba Januari 4 hilo halina ubishi. Ambacho hakijulikani ni kwamba watafungwa ngapi. Simba wamepania kushusha kichapo kizito kama kile cha 2012.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic