December 25, 2019


HATIMAYE straika wa Yanga, raia wa Burundi, Issa Bigirimana, ameomba kuachana na klabu hiyo kufuatia kutopata nafasi ya kukichezea kikosi hicho tangu aliposajiliwa.

Bigirimana aliungana na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akiwa na mwenzake, Patrick Sibomana, raia wa Rwanda ambaye yeye amekuwa na wakati mzuri ndani ya klabu hiyo tofauti na yeye ambaye tangu kikosi hicho kianze mechi za msimu huu, hajabahatika kuichezea hata katika mechi moja ya Ligi Kuu Bara.

Chanzo makini kimelieleza Championi Jumatano kuwa, Bigirimana ameamua kujitathmini mwenyewe na kuomba kuondoka baada ya kukosa nafasi ya kucheza tangu alipojiunga na mabingwa hao wa kihistoria.

“Naushangaa uongozi wetu, sijui kwa nini hautaki kuachana na Bigirimana ambaye mwenyewe anaomba kuondoka ili akatafute timu nyingine itakayoweza kumpatia nafasi nzuri ya kucheza, najua alisajiliwa kwa fedha nyingi lakini hilo halitufanyi sisi kukataa kumuacha maana kiukweli kwetu ameshindwa kutumika kama tulivyodhania,” kilisema chanzo hicho.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amethibitisha kuondoka kwa Bigirimana.

“Ni kweli Bigirimana aliomba kuondoka na sisi kama klabu hatukuwa na kipingamizi kwake, hivyo tayari alisharuhusiwa na kwamba hapa ninapoongea mimi nafahamu alishafika kwao kutafuta timu nyingine,” alisema Bumbuli.

Hadi sasa Yanga imeshaachana na wachezaji wake wapya wawili iliowasajili mwanzoni mwa msimu huu, ambao ni Juma Balinya na Sadney Urikhob na Maybin Kalengo tayari ameshatanguliza mguu mmoja nje.

3 COMMENTS:

  1. Msipotulia watani mtapata dharba kubwa sana tarehe 4.01

    ReplyDelete
  2. Tunaendesha timu na huku tumefumba macho

    ReplyDelete
  3. Ukikosa cha kuandika kuhusu Yanga blog haitasomwa? Bigirimana kaondoka Leo hadi uamue kuirudia tena hii story

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic