December 25, 2019


KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa wachezaji wake walipambana mbele ya timu bora kwenye fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Duniani dhidi ya Flamengo.

Liverpool Jumamosi usiku ilishinda kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Flamengo na kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa kombe la klabu bingwa duniani.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Roberto Firmino kwenye muda wa nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare tasa.

"Ni maajabu kuona namna gani wachezaji wangu wameshinda, walicheza na wachezaji ambao wana uwezo mkubwa jambo ambalo liliwafanya wapate taabu kupata matokeo mapema.

"Kwa sasa tuna ratiba ngumu kwani tuna mchezo dhidi ya Leicester City ambao ni wa ligi ila hakuna namna tutapambana," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic