Licha ya wachezaji wake kadhaa wa kimataifa kuandika barua za kuachana na Yanga, uongozi wa klabu hiyo umewataka wanachama na mashabiki wake kutokuwa na wasiwasi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli, amewaanbia wanayanga wote kutokuwa na wasiwasi sababu wamejiandaa kufanya usajili wa maana dirisha dogo.
Usajili ambao Yanga wanalenga zaidi kuufanya ni nafasi ya ushambuliaji ambay imeonekana kuwa na mapungufu zaidi.
Ameeleza wamedhamiria kufanya usajili wa maana kutokana na mwenendo wa timu namna ulivyo kiasi cha kwamba imepelekea kisiwe na matokeo mazuri katika siku za hivi karibuni.
"Nawaomba wanayanga wasiwe na wasiwasi.
"Kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya kufanya usajili wa maana kunako dirisha dogo.
"Tunalenga zaidi kuzingatia eneo la ushambuliaji ambalo linaonekakana kuwa na mapungufu mengi."








Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
ReplyDeleteUnajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup
Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji
1. Sadney Urikhob
2. Juma Balinya
3. Maybin Kalengo
Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikawa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa. Nadhani Simba Sports Club inaendeshwa kisayansi na kisasa zaidi na CEO mpya kuliko Yanga....wao wanaendesha kwa kisiasa na kiswahili!
Ahsanteni
Ungekuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira hasa Klabu ya Yanga ungepata picha ya nini kinachofanyika. Maybin Kalengo hajacheza mechi yoyote ya ligi hasa kwa kuanza direct, Juma Balinya alikuwa wa kuingia na kutoka na hakuwa na wakati mzuri katika ufanisi wake. Sidney Urkob alikuja kama msambuliaji lakin ukiangalia ni mvivu kweli uwanjani. Sasa hatuitaji mchezaji wa aina hiyo hata kama ametoka nje ya nchi yetu. Hata huko Simba unakokusema napo pia watafanya yao na mabadiliko yao. Usiangalie kwa jirani..angalia kwako
DeleteKaka umeongea kwa ufasaha zaidi,kwanini mtu anataka kufananisha nanasi na embe?
DeleteTumechoka sasa upuuzi wa Yanga...sitacomment tena...madudu na mambo ya ovyo ovyo yanayoendelea Yanga siyo tu yanahuzunisha bali yanasikitisha...timu inaendeshwa kama Lipuli...kama wako karne ya 18.....hakuna weledi na mambo yanaenda kiswahili swahili na viongozi ni wanasiasa hawana weledi na nia ya dhati kuipaisha timu...hakuna ambaye Ana utaalamu na mbinu za kuongoza klabu kisayansi....so sad very sad!!!.....Msola amepewa uanachama mwezi wa 4 INASADIKIKA NI SIMBA....SASA MOTO UNAWAKA KUMTAKA AJIUZULU
DeleteKumbukeni wakati mnawasajili zile mbwembwe zenu leo chali
ReplyDelete. Mbwembe za kumsajili Juma Balinya zilikuwa kubwa kwakuwa Simba wakimtaka na walitarajia makubwa Kutoka Kwake na sasa wamemtema kama shubiri
ReplyDeleteTumechoka sasa upuuzi wa Yanga...sitacomment tena...madudu na mambo ya ovyo ovyo yanayoendelea Yanga siyo tu yanahuzunisha bali yanasikitisha...timu inaendeshwa kama Lipuli...kama wako karne ya 18.....hakuna weledi na mambo yanaenda kiswahili swahili na viongozi ni wanasiasa hawana weledi na nia ya dhati kuipaisha timu...hakuna ambaye Ana utaalamu na mbinu za kuongoza klabu kisayansi....so sad very sad!!!.....Msola amepewa uanachama mwezi wa 4 INASADIKIKA NI SIMBA....SASA MOTO UNAWAKA KUMTAKA AJIUZULU
DeleteSimba haiendeshwi kiswahili inaendeshwa kiarabu lol!!
ReplyDeleteT u m e c h o k a a a a na hizo bwembwe zenu viongozi wa Yanga.. Halafu mje Tena kutuambia huyu hajazoea mazingirà kwa usajili mnaoufanya,hatutaki kusikia ama kuona haya tunayoyapiti. Mashabiki tumeumia sna.
ReplyDelete