December 12, 2019

2 COMMENTS:

  1. Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
    Unajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup

    Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji
    1. Sadney Urikhob
    2. Juma Balinya
    3. Maybin Kalengo
    Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
    Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikawa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
    Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa. Nadhani Simba Sports Club inaendeshwa kisayansi na kisasa zaidi na CEO mpya kuliko Yanga....wao wanaendesha kwa kisiasa na kiswahili!

    Ahsanteni

    ReplyDelete
  2. Tumechoka sasa upuuzi wa Yanga...sitacomment tena...madudu na mambo ya ovyo ovyo yanayoendelea Yanga siyo tu yanahuzunisha bali yanasikitisha...timu inaendeshwa kama Lipuli...kama wako karne ya 18.....hakuna weledi na mambo yanaenda kiswahili swahili na viongozi ni wanasiasa hawana weledi na nia ya dhati kuipaisha timu...hakuna ambaye Ana utaalamu na mbinu za kuongoza klabu kisayansi....so sad very sad!!!.....Msola amepewa uanachama mwezi wa 4 INASADIKIKA NI SIMBA....SASA MOTO UNAWAKA KUMTAKA AJIUZULU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic