December 13, 2019


Wakati tambo za watani wa jadi zikiwa zimeanza kushika kasi, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, amewatahadharisha Yanga kujipanga kuelekea mechi hiyo.

Simba itakutana na Yanga mwakani Januari 4 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake.

Kaduguda amewapa tahadhari Yanga kwa kuwaambia wamalize migogoro yao mapema ili waepuke kukutana na kichapo cha maana.

Amewaomba wawe na tahadhari kwani wao wanazidi kujipanga na akiwaomba endapo wakifungwa wasije kusema sababu tulikuwa na migogoro.

"Tunawaomba wenzetu wajiandae vizuri kwani sisi tuko katika maandalizi.

"Vema wakamaliza migogoro yao haraka ili baadaye wasije leta visingizio kuwa wamepoteza kwa kuwa hawako vizuri."

5 COMMENTS:

  1. Muheshimiwa umesema maneno ya maana hatutaki visingizio visivyokuwa na maana wala matokeo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa akili yako we kaduguda utaifunga yanga kiurahisi? mbona nyie mikia fc mnawashwa Sana subirini hiyo tar 4 muanze kufukuzana

      Delete
  2. Wewe mzee unaota ndoto za mchana, ww zungumzia mambo ya mikia fc achana na yanga bwana

    ReplyDelete
  3. ni kweli siendi hata taifa maana tunawekewa mimba ya mrija huongoz wa yanga wasengwa bumbafu

    ReplyDelete
  4. Kwani mmemsahau Kaduguda aliyedai pesa za chapati,mmemsahau Kaduguda akiwa Fat akateua timu kushiriki mashindano ya Afrika kwa matakwa yake kinyume na kanuni unayosema bingwa wa ligi na mshindi wa pili ndio washiriki halali michunuano ya Caf,lengo ilikuwa kuikomoa Yanga waliokuwa na haki kwa maelezo hayo mtumie kama kipimo cha akili yake,Simba ina viongozi wanaopaswa kupimwa akili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic