December 7, 2019

 OFISA Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' amesema kuwa ugeni walioupokea kutoka Hispania una manufaa makubwa ya kuongeza ushirikiano na timu ya Azam FC pamoja na Taifa kiujumla.

Jana Azam FC ilipokea ugeni kutoka kwa mwakilishi wa Ligi Kuu Hispania (La Liga) nchini, Alvaro Paya, ikiwa ni sehemu ya kutengeneza ushirikiano na klabu ya Real Betis ya huko.

Paya yupo nchini kwa muda wa miezi sita sasa, pia ni mwakilishi wa Real Betis moja ya timu kubwa nchini Hispania.

"Amejionea mwenyewe uwekezaji wetu wote, lakini kikubwa yeye pia ni mwakilishi wa klabu moja kule Hispania ya Real Betis, kwa hiyo Real Betis wao ndio wamemtuma pia hapa kuja kuangalia moja kwa moja uwekezaji ambao tunao hapa.


"Lakini kikubwa wao wanataka ushirikiano baina ya wao na sisi Azam FC, hasa Azam Academy na wao Real Betis, na amekuja yeye kwa ajili ya kutengeneza huo ushirikiano baina ya sisi na Real Betis," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic