MOHAMED Salah, mshambuliaji wa Liverpool alipachika bao la tatu na la mwisho kwa timu yake ya Liverpool wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Bournemouth.
Mchezo wa Leo ulikuwa ni wa kukata na shoka ambapo bao la kwanza lilipachikwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 35 kipindi cha kwanza na walitumia dakika 10 kuandika bao la pili kupitia kwa Naby Keita dakika ya 44.
Kipindi cha kwanza kilikamilika Liverpool ikiwa mbele Kwa mabao mawili huku wenyeji wao Bournemouth wakiwa hawana kitu.
Kipindi cha pili Liverpool ilipata bao moja pekee lililopachikwa kimiani na Salah ambaye aliukosa mchezo wa ligi dhidi ya Everton iliyochapwa mabao 5-2.
Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha jumla ya pointi 46 ikiwa kileleni baada kucheza mechi 16 za Ligi Kuu England.








0 COMMENTS:
Post a Comment