December 26, 2019


Kituo cha usalama kilichoko karibu na nyumba ya rais wa zamani wa Nigeria,  Goodluck Jonathan,  katika jimbo la Bayelsa, nchini Nigeria,  kimeshambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana na askari mmoja ameuawa.

Msaidizi wa Jonathan anayeshughulikia mambo ya habari amesema watu hao wenye silaha walifanya shambulizi kwa kutumia boti tano za injini dhidi ya kituo cha usalama kinacholinda usalama wa nyumba ya rais huyo wa zamani.

Habari pia zinasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres,  ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kuuawa kwa raia na kutekwa nyara na makundi ya watu wenye silaha kaskazini mwa jimbo la Borno, Nigeria.

Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu waliouawa, huku akisisitiza kuwa umoja huo uko pamoja na watu na serikali ya Nigeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic