December 25, 2019


HASSAN Dilunga, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa ushindi wa leo wa mabao 4-0 mbele ya Lipuli uwanja wa Uhuru ni zawadi ya mashabiki siku ya X-Mass na umetokana na umakini wa kutumia makosa ya wapinzani wao kupata matokeo.

Kwenye jumla ya mabao 4-0 ambayo Simba imefunga leo, Dilunga alifunga mabao mawili dakika ya 57 kwa mkwaju wa penalti na la pili dakika ya 65 akimalizia pasi ya Sharaf Shiboub huku lile la ufunguzi likifungwa na Francis Kahata akimalizia pasi ya Shomari Kapombe dakika ya 10 na la pili Meddie Kagere alipachika akimalizia pasi ya Clatous Chama.

"Tulikuwa makini katika kutumia nafasi ambazo tulizipata licha ya nyingine kuzikosa kutokana na ukweli kwamba mpira ni mchezo wa makosa ila kikubwa tumepata pointi tatu muhimu hilo ni jambo la kumshukuru Mungu na mashabiki kwa kujitokeza uwanjani," amesema.

Simba inajikita kileleni ikifikisha jumla ya pointi 28 ikiwa imecheza jumla ya mechi 11 kwa sasa na imeshinda mechi 9, sare moja na imepoteza mechi moja mbele ya Mwadui FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic