December 26, 2019


Mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba, amesema, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, alikuwa hajielewi wakati aliposema Alikiba lazima aimbe kwenye siku ya harusi yake.

Alikiba amesema hayo wakati alipoulizwa kuwa alikuwa anatoa ahadi gani baada ya Haji Manara kusema lazima alitakiwa aimbe kwenye harusi yake, na asipoimba au asipotokea kwenye harusi hiyo basi hata kama angekufa basi hakutakiwa kwenda kwenye msiba wake.

Alikiba amejibu kuwa: “Aliliongea hilo suala akiwa hajielewi, kiukweli, kwanza unajua katika harusi kukitokea vitu kama hivyo hata ndoa yako yenyewe inakuwa inakwenda kimuziki muziki tu, yeye alikuwa mwalimu wangu wa chuo cha dini, kwa hiyo aite watu wa madrasa wapige ubwabwa na maulid, mimi mwenyewe nitapiga dufu.”

Aidha ameongeza: “Lakini akitaka alete mambo yake ya watu kwenda kuimba haifai au twende kidini kama alivyokuwa akinifundisha mimi chuoni basi hata yeye apate matokeo yake pale.”

Manara ametangaza kufunga ndoa ifikapo mwaka 2020, ila hajasema itakuwa lini kwa sababu anaogopa watu akidai ‘watamroga’.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic