SHARAF Shiboub, kiungo wa Simba raia wa Sudan amesema kuwa aliamua kusoma masuala ya IT kwa kuwa ni kitu anachokipenda.
Shiboub amehusika kwenye jumla ya mabao mawili huku yeye akifunga bao moja kati ya 19 yaliyofungwa na Simba kwenye ligi.
Ni miongoni mwa wachezaji wasomi Bongo akiwa na degree kichwani kwa masuala ya IT aliyoipata nchini Sudan.
Shiboub amesema:-"Niliamua kusoma masuala ya IT Kwa kuwa ni kitu ambacho ninakipenda kutoka moyoni ndio maana nikafanya vizuri kwenye masomo haya.
"Pia inanipa nafasi kwamba siku nikiachana na soka nitafanya mambo mengine mbali na soka kwani maisha yana changamoto nyingi hivyo nikiachana na soka nitafanya kazi niliyosomea," amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment