PAPY Tshishimbi nahodha wa Yanga amesema kuwa, kaimu kocha Charles Mkwasa amewaelekeza jinsi ya kucheza bila kufungwa hivyo watapambana kufanya vizuri kwenye mechi zao zote.
Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi nana imefungwa mabao nane huku ikifunga jumla ya mabao 12 kwenye ligi.
Tshishimbi amesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kuona timu inafanya vema kwenye mchezo wao wa watani wa jadi dhidi ya Simba Januari 4.
"Kocha anatuelekeza jinsi ya kuzuia ili tusifungwe lakini pia sisi wachezaji tunazungumza ili tusifungwe kwenye mechi zetu zilizobaki kwa sasa.
"Tunajua tuna mechi nyingi ngumu ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba tunachokifanya kwa sasa ni kujiandaa kuwa bora muda wote," amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment