Mchakato wa mabadiliko ndani ya Yanga bado ni kitendawili kutokana na namna mwenendo mzima unavyokwenda.
Kiongozi, Mwanasheria na Mwanachama wa Yanga, Alex Mgongolwa, ameibuka na kusema yeye na kamati yake maalum inayohusika na kuratibu suala la mabadiliko bado hawajakutana na kamati ya utendaji.
Mgongolwa amezungumza kupitia Sport Court ya Wasafi FM akisema hawajakutana na kamati hiyo lakini wana mpango wa kukutana siku za usoni ili kujadiliana mambo muhimu ya kukamilisha suala hilo zito.
Juzi Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mshindo Msolla, alisema mchakato unaenda vizuri na kufikia mwezi Mei mwakani wanaweza kuwa wamekamilisha suala hilo.








Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
ReplyDeleteUnajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup
Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji
1. Sadney Urikhob
2. Juma Balinya
3. Maybin Kalengo
Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikawa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa. Nadhani Simba Sports Club inaendeshwa kisayansi na kisasa zaidi na CEO mpya kuliko Yanga....wao wanaendesha kwa kisiasa na kiswahili!
Ahsanteni
Ninapata tabu kuielewa club kubwa na konge kama Yanga kuwa na maelezo mengi kiasi hiki. Mara kamati mara mchakato unaendelea. Inamaana viongozi waliochaguliwa hawakuwa na weledi wa kuikabili hali mbaya ya kilabu? Waliingia wanajua fika wala si swala la kuelezea media ila ni kutafuta ufadhili wa kiwango kikubwa. Ubabaishaji haufai.
ReplyDelete