December 13, 2019


Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaka beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' kurejea mara moja kazini kwa mwajiri wake.

Taarifa zinasema kuwa mabosi wa Yanga waliamua kukata rufaa dhidi ya mchezaji huyo ambaye aliamua kugoma kutokana na kudai stahiki zake.

Dante ambaye aligoma naye alifungua kesi TFF akiomba alipwe fedha zake ambazo ni zaidi ya milioni 45.

Licha ya kushitaki, Yanga nao walikata rufaa ya kutaka wamalizane wao kwa wao na inaelezwa TFF wameamua arejee kazini ili wakamalizane wenyewe.

Tangu msimu huu uanze, Dante ameshindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa takribani robo tatu ya mechi ambazo imecheza msimu huu.

6 COMMENTS:

  1. Huu no ukandamizaji, Dante aliamua kushitaki TFF baada ya kukosa suluhu kwenye klabu , leo unamrudisha kulekule. Dante hapa kwa misimamo yake hawezi kurudi. Naona kabisa anavyoelekea FIFA

    ReplyDelete
    Replies
    1. suala sio ukandamizaji......sheria ndo zinaongea kaka......kama huna ufahamu japo kidogo na mambo ya kisheria basi ni vema ukakaa kimya au ukatafuta wenye ufahamu japo kidogo wa sheria wakuelekeze nini kimefanyika kuliko kuongea vitu usivyovifahamu halafu ukaonekana mjinga.

      Delete
  2. You can force the donkey to the river, but impossible to force him drink the water

    ReplyDelete
  3. Ha ha ha ha ha DANTE my brother nilikwambia,hiyo timu ya wananchi hata ufanye nini utadhulumiwa tu.

    ReplyDelete
  4. Mi nafikiri hilo suala ni gumu sana. Kama TFF ambao wangekuwa msaada kisha wamemwambia arudi mezani, nachofikiria arudi ili aweze kupata stahiki zake.

    ReplyDelete
  5. Shida ya TFF ni kujaa unazi wa simba na yanga, huwezi kuwa mchezaji ukawashitaki simba na yanga TFF halafu ukapewa haki, Dante aende FIFA/CAF

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic