Kocha wa zamani wa Gor Mahia na AFC Leopards, Zdravko Logarusic (pichani chini) amehusishwa na kutaka kurudi tena Simba ya Tanzania baada ya klabu hiyo kummwaga kocha wake, Mbelgiji Patrick Aussems. Imeelezwa.
Simba kwa sasa inasaka kocha baada ya kuachana na Mbelgiji huyo, ambaye anatuhumiwa kushindwa kuiwezesha timu hiyo kuwa na kiwango kizuri na wachezaji kutokuwa na nidhamu.
Kocha huyo Mcroatia anaweza kurudi tena Simba, ambayo aliwahi kuifundisha katika msimu wa mwaka 2013/14.
Logarusic mwishoni mwa wiki iliyopita alitimuliwa kutoka katika timu ya taifa ya Sudan baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019
Misri) na ile ya Chan 2020 nchini Cameroon.
Mfaransa Didier Gomes pia inaelezwa kuwa naye anatajwa kuziba pengo hilo la ukocha Simba. Mafanikio ya Gomes ni pamoja na kuiongoza klabu ya Rwanda ya Rayon Sport kutwaa taji la Ligi Kuu na timu ya Cameroon ya Coton Sport katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Pia aliiongoza timu ya Guinea ya Horoya, ambayo iliongoza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa mwaka 2019/20.
Simba, ambayo ni ‘nyumbani’ kwa nyota wawili wa zamani wa Gor Mahia, Meddie Kagere na Francis Kahata kwa sasa inaoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kucheza raundi 10.
Simba wawe makini katika mchakato wa kocha wao mpya. Ila kuna kocha huyu mmoja kama Simba watakuwa na uwezo nae na kama anapatikana basi Simba watajenga timu moja ya heshima barani Africa.ALEKSANDAR ROJIC.Ni bwana mdogo tu miaka 38 lakini ujuzi na uzoefu alionao unazidi umri wake. Alishakuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Serbia wakati wanakuja world cup South Africa na kama vile haitoshi alishakuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa Ghana hadi Afcon vile vile kwa hivyo analielewa soka la Africa vilivyo. Katika umri wake huo mdogo alishawahi kuteuliwa kuwa kocha bora mara kadhaa. Moja ya sifa yake kubwa ni mtaalamu wa mazoezi ya kujenga mwili vile vile .Ni kocha kijana mtaalamu mwenye kiu ya mafanikio na wakati mwengine huwa mtu unajiuliza vipi tunaishia kuteua makocha wasio na viwango hasa kwa timu yetu ya Taifa wakati wataalam wa mpira wamejaa tele ndani ya Dunia hii?
ReplyDeleteTuchukuwe mwalimu alieonesha ubingwa kwengineko na wala si Yule aliyetimuliwa Kwa kuboronga huko Sudan na huku atimuliwe tena na kulipwa Kwa kuvunja mkataba kama kocha Zahera anavowaandama watani
ReplyDeleteha ha ha, nyie watu wa majungu hamuwezi kukaa na makocha Assems mmemuundia zengwe mpaka kaondoka hapo labda aje matola tu mzee wa fitna, hamna jipya nyie
ReplyDeleteSimba bwana vilaza kweli mnamtoaje kocha ambaye anaonyesha mafanikio kwenye timu? mnatafuta wa bei poa hamna jipya
ReplyDelete