December 4, 2019


Beki anayekipiga Marekani na LA Galaxy II, Abdallah Shaibu 'Ninja' juzi Jumatatu alikuwepo dimbani Uwanja wa Taifa kuzishuhudia Yanga na KMC zilivyokuwa zikiambana.

Ninja ambaye aliwahi pia kuichezea Yanga ameibuka na kueleza kushangazwa na namna timu yake ya zamani namna ilivyoonesha kiwango dhaifu dhidi ya KMC.

Ameeleza kuwa Yanga ni timu kubwa na inapaswa kuonesha soka tofauti na wenzao sababu wachezaji wake walikuwa kama wamechoka.

"Si Yanga wala KCM, walicheza kwa kupooza sana, imeonekana kama wachezaji wamechoka pengine ratiba ya ligi inawabana, ila wanahitaji kujitofautisha na timu nyingine ili kuchukua ubingwa,"

"Wachezaji wazawa wajaribu kuwapa nafasi, kwani wanakuwa wanajua ligi ilivyo kuliko wageni ambao nimeona wanakwama kidogo," alisema Ninja.

Ninja amerejea nyumbani Tanzania kwa muda kufuatia kuwa na mapumziko ambapo ligi yao imesimama, kabla ya kurudi tena Marekani hapo baadaye kuendelea na kazi kama kawaida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic