December 5, 2019


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utapambana kupata matokeo mbele ya Iriga United kwenye mcheo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Desemba 20 uwanja wa Uhuru ili kutwaa kombe hilo.

Bingwa mtetezi wa kombe hli ni Azam FC ambaye alishinda mbele ya Lipuli kwa bao 1-0 na aliiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kwenye kila mchezo ni lazima wapate ushindi kwani ndio furaha ya uongozi na mashabiki.

"Tutakuwa nyumbani kuwakabili timu ya Iringa United FC,hii ni timu inayotokea mkoani Iringa.

"Mara zote kwenye mashindano haya kila mechi ni fainali,tunatambua kuwa kila mchezo tunapaswa kushinda kwani malengo yetu makuu ni kubeba kombe," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic