December 11, 2019


Kupitia idara ya mawasiliano Yanga, walieleza wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na aliyekuwa mchezaji wao Balinya kutokea Uganda, ambaye alisajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kabla ya msimu huu kuanza.

"Yanga tunamshukuru Balinya kwa huduma yake aliyokuwa akitoa alipokuwa akiitumikia klabu yetu lakini tunamtakia kila la heri katika maisha yake ya soka huko aendako kwani tunaimani anaweza kufanya vizuri," alisema idara ya habari na mawasiliano ya timu hiyo.

3 COMMENTS:

  1. Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
    Unajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup


    Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji

    1. Sadney Urikhob

    2. Juma Balinya

    3. Maybin Kalengo
    Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
    Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikiwa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
    Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa

    Ahsanteni

    ReplyDelete
  2. Huyu Balinya ndio aliletwa Yanga kuja kumfunika kagere? YANGA wameingizwa mkenge hapa. Tena wanayanga walijipiga kifua kuwa wameipiga bao Simba kwa huyu mchezaji? Simba wana watu makini.Simba ni taasisi kubwa na kama ingekuwepo kenya basi watanzania wote tungeisifu na kuizungumzia Simba kutokana na jinsi wa wakenya walivyo na uwezo wa kuvitukuza vya kwao

    ReplyDelete
  3. Huyu so ndio ilisemekana yanga walitupiga la kisigino? Mnapoteza hela tuu kwa kusajili wachezaji ambao simba walijaribu kuwafuata ila baada ya upembuzi wa kina wakaona hawafai. Ila ninyi mkaona hapa hapa muwaridhishe mashabiki wenu kwamba mmepiga la kisigino..kumbe mmejipiga wenyewe.. Urikhob amefanya trial simba akashindwa nyie kwa uvivu wa kutafuta wachezaji mkaona huyu ni moto wa kuotea mbali.. mmesajili mchezaji hawezi kufunga hata one against one na golikipa..Leo nawachana.. fanyeni kazi kwa makini mkijisimamia.. by Eng.Elibarick Andrew.. msimbazi damu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic