December 7, 2019


Mabosi wa Yanga wamekiangalia kikosi chao kilichocheza michezo nane ya Ligi Kuu Bara, fasta wakakubaliana kushusha kiungo fundi mchezeshaji mwenye uwezo wa kuchezesha timu na kutengeneza mabao zaidi ya viungo wa Simba, Jonas Mkude na Mzamiru Yassin.

Safu ya kiungo ya Yanga hivi sasa inaongozwa na nahodha mkongwe Mkongomani Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Abdulaziz Makame ‘Bui’ na Issa Mohamed ‘Banka’.

Yanga imepanga kukifanyia maboresho kikosi chake kwenye usajili wa dirisha dogo baada ya wale waliowasajili kwenye usajili mkubwa kushindwa kuonyesha viwango vyao huku kati yao wakipangwa kusitishiwa mikataba yao.

Yanga wanataka kumsajili kiungo huyo mchezeshaji kutokana na nusu ya viungo waliopo kuwa ni wakabaji tofauti na Balama ambaye ndiye tegemeo hivi sasa katika timu.

Mtoa taarifa huyo alisema katika michezo yao waliyoicheza, timu imeshindwa kucheza kutokana na viungo wengi waliopo ni wakabaji akiwemo Tshishimbi ambaye ametumika katika michezo kadhaa kucheza namba 10 kabla ya kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa kumhamishia namba 6.

“Tshishimbi alikuwa analazimishwa kuchezeshwa namba 10 katika michezo ya ligi ni kutokana na kutokuwepo kiungo mchezeshaji mwenye uwezo wa kuchezesha timu, pia kutengeneza nafasi za kufunga mabao.

“Kiungo huyo alikuwa akichezeshwa kimakosa, Tshishimbi kiuhalisia ni kiungo mkabaji na siyo mchezeshaji na mkabaji, hivyo uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi wamekubaliana kusajili kiungo mwingine mmoja mchezeshaji.

“Hivyo, uongozi umemuachia Mkwasa suala hilo la kupendekeza kiungo mchezeshaji anayemuhitaji yeye na kikubwa katika kuisuka Yanga itakayokuwa imara,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo alisema: “Kamati ya Ufundi na Mashindano pamoja na kocha Mkwasa bado hawajakutana, hivyo ni ngumu kuliweka wazi hilo, tusubirie muda ukifika tutaweka wazi.”

4 COMMENTS:

  1. Msipoteze lengo tengezeni uwanja kama wenzenu Simba....bakuli halitawafikisha popote!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kamwambie mzee wako na lile msuli wake!

      Delete
  2. Maneno, siasa, porojo na hadaa tu....HAKUNA VITENDO BLAH BLAH ....MICHAKATO, MIKAKATI NA MIPANGO KWENYE MAKARATASI..HAKUNA VITENDO NI UPUUZI....WATU WAMEWACHOKA!!!!Msipoteze lengo tengezeni uwanja kama wenzenu Simba, msijivutevute na kusuasua.........bakuli halitawafikisha popote...tafuteni wawekezaji wawili au watatu wenye uwezo muingie ubia na makubaliano uwanja ujengwe!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic