January 31, 2020


MWAKA 2020 utakuwa wenye anguko kubwa kwa mastaa wa Bongo, habari mpya kutoka kwa mtabiri maarufu, Afrika Mashariki na Kati, Maalim Hassan Yahya Hussein zinaeleza. 

Risasi Mchanganyiko lilifunga safari hadi zilipo ofisi za mnajimu huyo maarufu, ambaye ni mrithi wa baba yake, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Magomeni – Mwembechai, jijini Dar na kufanya naye mahojiano marefu kuhusiana na utabiri wa mastaa Bongo.

Katika mahojiano hayo, Maalim Hussein ameeleza utabiri wake katika maeneo kadhaa ikiwemo vifo, mafanikio ya wasanii, mahusiano na mengineyo.

SAYARI YA VENUS

Wakati akianza kutoa utabiri wake, Maalim Hassan alisema, mwaka huu kinyota unatawaliwa na sayari ya Mekyuri (Mercury) na Mwezi (Moon).

Lakini kwa upande wa wasanii na sanaa kwa jumla, nyota inayotawala ni Ijumaa ambayo ni maarufu zaidi kama Venus inayohusisha sanaa na watu waliojipatia umaarufu kutokana na kazi zao.

“Kinyota huu ni mwaka wa sayari ya Ijumaa, ambayo zaidi inajulikana na watu wengi kama Venus. Hii ni sayari ya watu wanaojihusisha na sanaa na wale maarufu kupitia kazi mbalimbali,” anaanza kueleza Maalim Hassan.
MASTAA ANGUKO

Miongoni mwa mambo makubwa ambayo Maalim Hassan ametabiri ni kuwepo kwa anguko la wasanii wakubwa hapa Bongo (na duniani) ambao tayari wamezoeleka na wameshika vichwa vya habari kwa muda mrefu. Bila kueleza aina ya fani za wasanii hao, amesema mastaa hao ambao wanawika kwa sasa, watashuka na nafasi zao zitachukuliwa na wasanii ambao wanaonekana kuwa chini.

Baadhi ya mastaa wanaowika kwa sasa ni pamoja na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Ali Saleh ‘AliKiba’, Vanessa Mdee, Faustina Mfinanga ‘Nandy’, na Yusuf Mbwana ‘Mbosso’ wote kutoka muziki wa Bongo Fleva. Kwa upande wa filamu, mastaa wanaowaka ni Daudi Michael ‘Duma’, Salim Ahmed ‘Gabo’, Yvonny Cherry ‘Monalisa’, Jacob Stephen ‘JB’, Wema Sepetu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Mussa Kitale ‘Mkude Simba’ na Riyama Ally.

MAFUMANIZI

Akiendelea kutabiri ameeleza kuwa katika nyota hiyo ya utabiri juu ya wasanii, inaonyesha kutakuwa na kashfa nzito za ngono ikiwemo kukithiri kwa mafumanizi yanayohusisha wasanii na mastaa wakubwa. “Nyota hii inaonesha kuwepo kwa kashfa za ngono, ikiwemo wasanii wakubwa kufumaniwa, jambo litaloshusha thamani ya kazi zao,” alisema Maalim Hassan.

MAHUSIANO KUTIKISIKA, NDOA KUVUNJIKA

Maalim Hassan anaeleza, kutokana na mafumanizi na migogoro kwenye uhusiano, wengi wataachana katika uhusiano wao huku wengine wakiamua kuvunja ndoa zao. “Siyo mwaka mzuri kwa wasanii wakubwa, kwani pia utabiri unaonesha kuwa ndoa na mahusiano mengi yatavunjika kutokana na sababu mbalimbali na hasa nilizoeleza awali – migogoro na kufumaniana,” alisema.

VIFO

Hakuishia hapo, alieleza kuwa kwa mwaka huu utabiri unaonesha kutakuwa na vifo vya wasanii maarufu, akieleza kuwa vitakuwa vya ghafla. Hata hivyo, alisema idadi ya wasanii watakaoaga dunia mwaka huu itapungua tofauti na mwaka jana.
TAHADHARI YATOLEWA

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kuhusiana na utabiri huo, mchungaji wa kanisa moja jijini Dar (ameomba hifadhi ya jina lake), ametoa neno kwa mastaa nchini.

“Mimi ni mtumishi wa Mungu, siwezi kueleza mambo ya kinajimu, lakini ninachofahamu mtu akiishi maisha safi, anajiweka mbali na hatari mbalimbali. Kwa mfano umeniuliza kuhusu fumanizi na ndoa kuvunjika, inaeleweka wazi, mtu anayetulia katika ndoa yake, hawezi kukutwa na kadhia za namna hiyo.

“Ukiniambia kuhusu kushuka kisanii, nitasema msanii akifanya kazi iliyo bora, yenye ubunifu, akamtolea Mungu sadaka na kuwasaidia wajane na yatima, ataendelea kuwa juu. Huo ndiyo ukweli,” alisema mchungaji huyo na kuongeza:

“Kuhusu kifo, ninachoweza kusema ni kwamba kifo ni ahadi. Ndiyo maana hata barua ya Paulo Mtume kwa 2 Timotheo 4:7, anaeleza: ‘Nimepigana vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda’. Muhimu hapo ni kuilinda imani na kuwa tayari kwa wakati

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic