January 5, 2020


KOCHA Mkuu wa Wolves, Nuno Espirito Santo amesema kuwa mshambuliaji wake Raul Jimenez anaweza kusepa ndani ya klabu hiyo mwezi huu na kujiunga na Manchester United.
Habari zinaeleza kuwa Manchester United wanahitaji saini ya nyota huyo ambaye amekuwa kwenye ubora wake ili kuongeza ukali wa safu yao ya ushambuliaji.
Raia huyo wa Mexico alitokea benchi kwenye mechi ya FA jana, Jumamosi ambapo Wolves ililazimisha sare ya bila kufungana mbele ya United raudi ya tatu.
Jimenez amefunga jumla ya mabao 17 na pasi tisa za mabao kwenye jumla ya mechi zake zote 32 alizocheza akiwa na Wolves kwenye mashindano yote msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic