January 7, 2020


MWAMUZI mwenye beji ya Shirikisho la Sola la Kimataifa (Fifa), Omar Abdulkadir, amesema penalti waliyopewa Simba na kuzaa bao la kwanza lililofungwa na Meddie Kagere haikuwa halali.

Lakini mwamuzi mwingine mwenye beji ya Fifa, Othuman Kazi yeye amekuwa na mawazo tofauti akisema ilikuwa ni penalti halali.

Kumekuwa na mjadala mkubwa kama penalti ile ni halali au la baada ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2 Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba ilipata penalti katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza baada ya beki wa Yanga Kelvin Yondani kumvuta mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kabla ya mwamuzi wa mchezo huo Jonesia Rukyaa kuweka penalti ambayo ilifungwa na Kagere.

Abdulkadir ambaye alistaafu mwaka 2004 akiwa na miaka 45, alisema kuwa kwa upande wake anashindwa kukubaliana kuwa ilikuwa penalti kwa sababu zake tatu alizozitoa huku Kazi yeye akiamini ilikuwa penalti halali.

Abdulkadir alisema kuwa sababu yake ya kwanza ilinayompa ugumu kuamini ilikuwa penalti ni kwa kuwa mwamuzi hakuwepo katika eneo la tukio lakini akaenda mbali zaidi kwa kumtupia lawama mwamuzi msaidizi namba moja, Soud Lila kwa kushindwa kutafsiri tukio hilo.

“Kuna mambo matatu ambayo yananipa ugumu kusema ninachokiona labda ningekuwa nimeangalia tena lakini kwa tukio lilivyotoa mwamuzi alikuwa mbali, sasa sijui kwa nini alisema penalti au alionaje.

“Pili, mwamuzi namba moja yeye ndiyo alipaswa kujua kwamba ilikuwa penalti kwa sababu alikuwa karibu na tukio ila alishindwa kusema kitu na mwisho ukiangalia naona tukio limefanyika nje kabisa ya 18, sasa sijui kipi ambacho kimepelekea hivyo,” alisema Abdulkadir.

Lakini kwa upande wa Othuman Kazi alisema kuwa anaamini penalti ilikuwa sahihi na halali kutolewa na mwamuzi kwa kuwa beki wa Yanga alifanya kosa akiwa tayari ameshakanyaga mstari wa eneo la 18.

“Kisheria naona mwamuzi alikuwa sahihi kutoa ile penalti kwa sababu tukio limetokea wakati wameshakanyaga mstari wa eneo la 18, hivyo alichokiamua kilikuwa sahihi kabisa,” alisema Kazi wakati alipokuwa akichambua tukio hilo kwenye kituo cha Azam TV.

Championi lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Chama ambaye alisema kuwa kwa upande wake anawapongeza waamuzi wake kwa kuwa walichezesha bila ya upendeleo wowote licha ya kuwa na upungufu wa kibinadamu.

“Binafsi naona waamuzi wangu wamechezesha vizuri lakini nawapa alama 95 katika mchezo ule na alama tano ni za makosa ya kibinadamu ambaye mtu yeyote anaweza akafanya.

“Unajua huwezi kufanya kila kitu kikawa sawa ndiyo maana wenzetu Ulaya wanatumia teknolojia ya VAR kwa ajili ya kusaidia kutoa maamuzi kwenye matukio tata lakini kwa Afrika bado kutokana na changamoto ya kiuchumi katika mashirikisho yetu,” alisema Chama.


14 COMMENTS:

  1. Hakuna cha kuandika zaidi ya penati hakuna mengine?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nahisi hakuna. Hakuna cha ajabu trend kama inajirudia mechi ya kwanza droo ya pili Yanga anafungwa. Hii ni kwa misimu miwili iliyopita.

      Delete
  2. OTHMAN KAZI UNAPOTEZA IMANI KWA SISI TULIOKUA TUNAKUAMINI MAANA KILA KITU KILIONYESHA
    KUA FAULO ILIFANYIKA NJE YA MSTARI

    ReplyDelete
  3. Othmani Kazi anapotosha watu ila huo ni mtazamo wake
    Ukweli utabaki pale pale ile haikuwa Penalt halali

    ReplyDelete
  4. Ila imekwishapigwa!!!!

    ReplyDelete
  5. sasa kama mwamzi mmoja wa fifa amesema penalty ni halali na huyo mwingine kasema sio halali ndiyo unaandika kuwa penalty imekataliwa kwenye kichwa cha habari? kumbuka waamuzi wawili walikubaliana ni penalty halali. Mkiandika kuwa waamuzi wametoa penalty sio halali andikeni basi na kuwa Yondani alipaswa kupewa kadi nyekundu. Acheni ushabiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kadi nyekundu haijadiliwi kabisa. Inaonekana Yanga wananguvu sana katika media. Wanajadili penalti tu.

      Delete
  6. Mpira wa bongo bwana!!!!Ingekuwa wenzetu katika nchi zilizoendelea katika soka mjadala kwa mashabiki,viongozi wachezaji na benchi la ufundi ungekuwa umefungwa siku ile ile ya mechi lakini hapa kwetu imekuwa ni story kila mtu anataka aongee na kuandikwa au kusikika kwenye vyombo vya habari

    ReplyDelete
  7. Biashara ya magazeti kwani akili za wahariri wetu zimeozeana kunako uvivu kutafuta habari wanabaki kudakia matukio wakiyarejea kuyachapisha hayo kwa hayo.

    ReplyDelete
  8. Huu mjadala wa penalty ufungwe sasa. Mpira umekwisha, Mimi binafsi nisingependa kumlaum refa. Tukumbuke hata marefa pia wana presha kubwa sana wanapochezesha mechi ya watani wajadi, kwa hiyo makosa mengi hutokea kwa sababu ya presha. Suluhisho TFF watumie VAR kwenye mechi kubwa kama inawezekana.

    ReplyDelete
  9. Wewe mwandishi mpumbavu na huyo mzee anayekataa penati ni mjinga....sasa kama anakubali kuwa faulo ilichezeka ila ni nje ya 18 kwanini hazungumzii kutokupewa kadi nyekundu kwa yondani kwasababu alikuwa ni mtu wa mwisho????


    Wapumbavu watupu nyie

    ReplyDelete
  10. Othman kazi pale azam sport a am hakusema kwamba ilikua penalty Bali alisema HAIKUA penalty ila Yondani alistahili RED card kwakua kagere alikua mtu wa mwisho.

    ReplyDelete
  11. Back to school ukajifunze kuandika heading

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic