January 27, 2020


ALLY Ally, beki wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kuibukia kwenye Klabu yake ya zamani KMC  kwa mkopo na sio kwenda kwenye timu nyingine ikishindikana atabaki Yanga.

Ally alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha kubwa kwa kandarasi miaka miwili akitokea KMC, kwa sasa uongozi wa Yanga umepanga kumtoka kwa mkop kwenda JKT Tanzania jambo ambalo ameligomea.

"Sipo tayari kwenda kwenye timu nyingine kwa sasa, labda nirudi KMC hapo nipo tayari ila sehemu nyingine hapana siwezi kwenda," amesema.

Jamila Mutabanzi, Ofisa Habar wa JKT Tanzania aesema kuwa Ally alipaswa ajiunge na wenzake kwenye mazoezi ila bado hajatokea.

"Tulipewa barua na Yanga kwamba wanataka aje kwetu kwa mkopo, suala la yeye kugoma hilo wanapaswa wamalizane ndani ya Yanga," amesema.

4 COMMENTS:

  1. YANGA wajinga wanasajili mchezaji kwa ajili ya mechi ya simba na ikitokea amefanya vyema kwenye mechi ya simba basi mchezaji lakini mchezaji huyo akishindwa kufanya vizuri kwenye mechi ya simba basi si mchezaji. Huyu Ali Ali Yanga walimsajili kwa tambo na vibweka kisa alicheza vizuri kwenye timu yake ya zamani ilipokutana na Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Enter your reply...huo ndo uongo alikwambia nan hizo habar ,Ally anaondolew kutokana na kushehen wachezaj wengi kwenye nmba yake ko wameona wamtoe kwa maslahi yake kimpira,hayo ya simba ni kweli ila ni mawazo yako kiushabiki,kwan nyie mlimsajir salamba kwaajir ya Yanga ??????

      Delete
  2. Salamba alipata muda wa kutosha wa kukitathmini kiwango chake ndani ya kikosi cha Simba na hajatolewa kwa mkopo au kuachwa bali aliamua kwenda Kuwait falme za kiarabu na hivi sasa anaoga mihela maradufu ya yale aliokuwa akiyapata Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic