STRAIKA wa Paris Saint German, Kylian Mbappe, kwa sasa anaangalia nini anatakiwa kufanya ndani ya klabu hiyo na mwisho wa msimu atajua anaelekea wapi.
Mbappe amekuwa akiwindwa na klabu nyingi za Ulaya ikiwemo Real Madrid na Liverpool ambazo zinaonekana kama kukomalia zaidi dili la staa huyo.
Staa huyo mwenye miaka 21, amekuwa na kiwango bora hali inayozifanya klabu kadhaa kumtolea macho.
Mbappe ameeleza kuwa, hivi sasa anaangalia zaidi timu yake kuona inafanya nini na mwisho wa msimu ndiyo atajua hatma yake.
“Kila mtu kwa sasa analizungumzia suala langu, mimi ni mchezaji, kwa sasa nasubiri tu wakati ufike.
“Nataka kutwaa makombe mengi ili kuisaidia timu yangu kufika mbali zaidi ya hapa tulipo sasa, lakini kuhusu hatma yangu ni mapema, tusubiri mwisho wa msimu ndipo tunaweza kuzungumza.
“Kwa sasa naifikiria klabu ambayo imenisaidia, nakumbuka nilikuja hapa nikiwa na miaka 18 na sikuwa staa, lakini leo hii ni staa, naishukuru sana PSG na timu ya taifa ya Ufaransa,” alisema Mbappe.
Kichwa cha habari kimemtaja Neymar lakini taarifa iliyoko ndani inamtaja Mbappe..Imekaaje hii?
ReplyDelete