ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amemuangalia straika Muivory Coast, Yikpe Gnamien ambaye Yanga wanatamba naye, akasonya kwa sauti na kukunja sura kama mtu aliyekutana na pilipili kichaa bahati mbali kwenye pilau.
Yanga katika usajili wa dirisha dogo imesajili nyota sita wakiwemo wachezaji wa kigeni ambao ni Yikpe ili kuziba nafasi za wachezaji waliowaonyesha mlango wa kutokea.
Julio ambaye ni Simba kindakindaki, alisema kuwa, kiwango kilichoonyeshwa na Yikpe katika mechi alizocheza hakikumfurahisha hata kidogo na kudai kuwa ni bora nafasi hiyo akapewa mzawa.
“Yikpe unaona kabisa haendani na kiwango cha Yanga, ni vyema wanaokwenda kuchagua wachezaji maprofeshno lazima waangalie historia zao katika timu za taifa iwapo wanachezea ndipo waweze kuwapa nafasi ya kusajiliwa,” alisema Julio.
YANGA Kwa makelele ya mitaani juu ya timu yao wamefanikiwa kwa hilo ila timu hawana kinachowabeba ni jina tu.Tulipigiwa kelele kuhusu juma Balinya sijui mzambia kalengo ila hakuna lolote ujinga mtupu.
ReplyDeleteHahahahaaaa! Achana na Yanga,nyie marefa wakuwabeba wapo
ReplyDeleteMe nashaangaa simba kazi yenu kuifuatilia yanga maboya nyie
ReplyDeletehata sku moja sjawahi ona App Simba ikiandika malalamiko kuhusu yanga kushinda kwa kupendelewa mfano:
Deletegoal vs coastal u
ofside ya molinga
na nyingne nyingi
Sasa nenda nenda App ya vyura duuh kila asubuhi lazma wawe na story ya kuizodoa simaba