January 29, 2020

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba leo amewanyanyua mashabiki wa timu yake kwa kufunga bao la ushindi lililoipa timu yake pointi tatu mbele ya Namungo FC.

Simba leo ilikuwa ikicheza Uwanja wa Taifa na ilianza kujipatia bao dakika ya 21 kupitia kwa Francis Kahata aliyefunga bao hilo dakika ya 21 lililosawazishwa na Bigirimana Blaise dakika ya 35 na Hassan Dilunga akafunga bao la pili akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Balora na kuwafanya Simba kuenda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili Namungo walipata bao la pili kupitia kwa Lusajo ambaye aliachia shuti kali akiwa nje ya 18 alichoambulia Kakolanya ilikuwa kuokota mpira nyavuni.

Dakika ya 88, Kagere alimaliza shughuli uwanjani kwa kufunga bao la ushindi ambalo limewapa Simba pointi tatu jumla.

Sasa inafikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya kwanza na imefunga jumla ya mabao 38.

9 COMMENTS:

  1. Goli la tatu Ni Off side ya wazi...sijui mshika kibendera alilala.. .

    ReplyDelete
  2. Beki kamkimbia Kagere ili awe offside.Angalia pass ya Shibob inapopigwa ndio utajua .Wacha kulalama bila kujua sheria ya offside .

    ReplyDelete
  3. Amemaliza kazi kwa zawadi ya goli alilopewa na refa, marefa tanzania ni kichefuchefu,

    ReplyDelete
  4. Povu ruksaa,kilichobakia ni history kwani licha ya Yanga kucheza nyuma ya Mgongo wa Namungo mnyama kaondoka na points muhimu.

    ReplyDelete
  5. Kama unasikia kichefuchefu kanunue ndimu inawezekana ni mimba changa.

    ReplyDelete
  6. Heeheeehee mimba changa nimecheka kwa volume yaan hawa vyura wao kazi nikutafuta kosa la simba tu ila ya kwao hawayaoni sku molinga anafunga goli la offside tena kwa mkono sikuona kelele za hivi

    ReplyDelete
  7. Jamani mmesahau? Yanga huwa hakosei ila anaonewa tuuuu

    ReplyDelete
  8. Picha za video za marudio zinamuonesha beki wa Namungo akimkimbia Kagere wakati mpira umeshapigwa. Kwa vyovyote vile ile haiwezi kuwa off side. Sheria ya off side ipo very clear kuhusu hilo na ndio maana waamuzi wale wenye badge ya Fifa walilikubali goli la Kagere.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic