SVEN Vanderboeck raia wa Ubelgiji, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wanashindwa kutumia nafasi wakiwa ndani ya 18 jambo ambalo linawapa ugumu kupata matokeo.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 44 jana, Januari 29 Uwanja wa Taifa ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Namung FC.
Sven amesema :"Wachezaji wangu bado hawajafikia ile hatua ya kutumia nafasi ambazo wanazitengeneza kwani wakifika ndani ya box wanashindwa kufunga jambo linalotokana na kukosa umakini na utulivu.
"Nitaongea nao ili kujua ni namna gani tunaweza kulimaliza tatizo hili kwani linazidi kuleta ugumu kutupatia matokeo,".
Sasa hapo amewaka vipi?
ReplyDeleteKwa upeo wa mwandishi ndo amewaka hivyo??????
ReplyDeleteHuyo mwandishi ni kandambili
ReplyDelete