MBWANA Samatta, nyota mpya wa Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England amesema kuwa kwa hatua aliyofikia ni suala la kushukuru Mungu huku akiahidi kuendelea kupambana.
Samatta anakuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kubwa ya England kwa kusaini kandarasi ya miaka minne na nusu akitokea Genk alikokuwa anakipiga awali.
'Ninashukuru Mungu kwa hatua ambayo nimefikia kwa sasa, sapoti ya mashabiki na maombi ya watanzania kiujumla yananifanya niwe hapa nilipo.
"Kwa maombi yenu ndugu zangu ninawashukuru ila mapambano yanaendelea," amesema.
Samatta ataukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Watford kutokana na utaratibu wa Ligi ya England kuwasilisha kikosi kitakachocheza masaa 15 kabla ya mechi husika.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alianzia kucheza soka la ushindani Simba na kujiunga na TP Mazembe aliibukia Genk mwaka 2016 amefunga jumla ya mabao 76 kwenye mechi 191 ndani ya Genk na mabao 18 kwenye mechi 51 kwenye timu ya Taifa ya Tanzania.
Hongera sana Samatta, Mungu azidi kukuangazia ktk mafanikio ya kweli.
ReplyDeleteHayo ndio mafanikio kunawengine wanafurahia mchezaji akirudi bongo kwavile atawafunga wapinzani wao, kaazi kweli kweli