SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameonekana kumpa shavu kipa namba mbili Beno Kakolanya huyo kuanza katika michezo sita kati ya michezo kumi ambayo amekiongoza kikosi hicho baada ya kupewa mikoba ya Patrick Aussems.
Katika michezo hiyo tisa, Kakolanya amewafunika makipa wenzake wa Simba,Aish Manula ambaye katika michezo tisa amefanikiwa kuanza katika michezo mitatu,huku kipa Ally Salim akifanikiwa kuanza katika mchezo mmoja pekee.
Kocha Sven alimuanzisha Beno katika mchezo dhidi ya Arusha FC wa kombe la FA, Lipuli FC mchezo wa ligi, Azam FC na Mtibwa Sugar katika kombe la Mapinduzi na dhidi ya Mbao na Alliance zote za ligi.
Aishi Manula alianza katika mchezo dhidi ya KMC ,Ndanda na ule wa watani wa jadi dhidi ya Yanga ambayo yote ikiwa ni michezo ya ligi ,huku kipa Ally Salim akianza katika mchezo mmoja pekee ule wa kwanza wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Zimamoto.
Aidha katika michezo sita ambayo Kakolanya ameanza,Simba imefanikiwa kupata ushindi katika michezo minne huku akipoteza mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa kwa bao 1-0, suluhu dhidi ya Azam michezo yote hiyo ikiwa katika kombe la Mapinduzi.
Aidha kipa Manula katika michezo mitatu aliyocheza amefanikiwa kuondoka na ushindi katika michezo miwili huku mmoja Simba ikitoka sare dhidi ya Yanga kwa mabao 2-2,huku Ally Salim akiipatia ushindi Simba katika mchezo mmoja alioanza dhidi ya Zimamoto.
Awali kocha aliyeondoka hivi karibuni katika kikosi hiko Patrick Aussems alikuwa akimtumia sana golikipa Aish Manula katika kikosi cha kwanza kuliko Beno Kakolanya ambaye alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara chache zaidi,ambapo kwa sasa kocha Sven ameonekana kumtumia zaidi kipa Beno Kakolanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment