HASSAN Dilunga 'HD' alianza kupeleka maumivu kwa wapinzani wao leo Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba kwa kufunga bao la kuongoza dakika ya 44 akimalizia pasi ya Jonas Mkude.
Bao hilo liliwapeleka Simba mapumziko wakiwa mbele huku Mbao FC wakienda kujipanga kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa leo ambao ulichezwa kwenye Uwanja wenye maji kutokana na changamoto ya mvua.
Kipindi cha pili Mbao iliyo chini ya Hemed Moroco walijipanga upya kabla ya kuanza kuonyesha kasi yao Jonas Mkude aliongeza uzito kwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu kwa shuti kali akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu na kuwafanya Simba kuwa mbele kwa mabao 2-0.
Mbao FC hawakuwa wanyoge walirejea mchezoni na dakika ya 52 alifunga bao la kufutia machozi akiwa katikati ya mabeki wa Simba na kuwarejesha kwenye mchezo Mbao.
Licha ya Mbao kufanya mashambulizi ya mara kwa mara haikuwa rahisi kupenya kwenye ngome ya ulinzi iliyokuwa chini ya Beno Kakolanya mlinda mlango namba mbili wa Simba.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 38 ikiwa nafasi ya kwanza ndani ya ligi kwa sasa ikiwaacha wapinzani wao Yanga 13 ikiwa imecheza mechi 13 na ina michezo miwili kuwa sawa na Simba kwa sasa ina pointi 25.







This is simba
ReplyDeleteLakini hawa watu wa bodi ya ligi ni wagonjwa wa akili ama vipi? Kwa nini Yanga wanaendelea kuishi na viporo hadi ligi inamalizika? Kwanini wasifanye utaratibu kuhakisha Yanga wanamaliza viporo vyake kwanza ili kuleta uwiyano sawa wa mechi na timu nyengine.
ReplyDeleteWakipangiwa wacheze si wataanza kulalamika wanacheza mfululizo .Kila mtu ashinde mechi zake.
ReplyDeleteNa kila wanapoona wanapitwa kwa point inazidi kuwatia kinyongo
ReplyDeleteNa kila Yanga wanapoyaona hayo hukurupuka Bila ya plan kuleta wapya. Jamaa wwanaona kuzunguzungu
ReplyDelete