January 14, 2020


BARCELONA imefika hatua ya makubaliano ya kuachana na Ernesto Valverde aliyekuwa Kocha Mkuu wa tImu hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake ndani ya kikosi hicho.
 Licha ya kocha huyo wa Barcelona kuiongoza klabu hiyo kuwa  vinara wa La Liga bado mabosi wake hawaamini uwezo wake kwa sasa.
Kusepa kwa bosi huyo kunatoa nafasi kwa kocha mkuu wa zamani wa Watford, Quique Setien kutwaa mikoba yake ambapo inaelezwa kuwa amepewa kandarasi ya miaka miwili baada ya mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Xavi aliyekuwa akitajwa kuibuka Barcelona kugomea dili hilo.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Barcelona imesema kuwa inashukuru kwa mchango mkubwa uliotolewa na Valverde kwa kuonyesha uwezo wake na kujitoa kwa ajili ya timu hiyo na alidumu kwa miaka miwili na nusu kwenye majukumu yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic