January 14, 2020

NEVER Tigere,kiungo aliyekuwa akikipiga ndan ya FC Platinum ya Zimbabwe amesaini kadnarasi ya mwaka mmoja.

Tigere ni pendekezo la benchi la ufundi la Azam FC, ambalo lilimfuatilia kwenye mechi kadhaa alizoichezea Platinum katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Nyota huyo anayemudu kucheza namba sita, nane na saba, hadi anaondoka Platinum amefanikiwa kuifungia mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo iliingia hatua ya makundi ya michuano hiyo mwaka huu.

Zoezi la kumwaga wino limesimamiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', huku wakala wake, George Deda akishuhudia.

Huo ni usajili wa pili kwa Azam FC kwenye dirisha dogo la usajili, wa kwanza akiwa ni kiungo mshambuliaji, Khleffin Hamdoun kutoka Mlandege.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic