MIONGONI mwa sababu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kulifanya soka letu lizidi kudidimia kila kuchao.
Wiki kadhaa nyuma niliandika makala kuhusu baadhi ya waamuzi kuchezesha soka bila kufuata kanuni 17 za soka kuna watu walinitumia ujumbe mfupi na niliposoma nilihisi ni kati ya waamuzi moja kwa moja maana wapo walionijia juu na kusema kuna waamuzi hawajalipwa kwa muda mrefu, nikajiuliza sana kuhusu hilo.
Kama wamekubali kuchezesha bila kulipwa kwa wakati maana yake wamekubaliana na hali halisi basi waitumie hiyo fursa kwa kuchezesha vyema ili wapate nafasi ya kwenda nje kuchezesha mechi za kimataifa.
Kumekuwa na maamuzi tata sana msimu huu hata ile iliyopita. Hii imesababisha hata majuu baadhi ya ligi kutumia VAR ambayo inamsaidia mwamuzi kwenye maamuzi yake.
Sawa waamuzi nao ni binadamu lakini utaona makosa mengine ni ya wazi kabisa lakini hawachukui hatua na wengine hupendelea upande fulani. Itatuchukua muda kuona nuru ya soka letu.
Inawezekana maamuzi mbalimbali tatanishi, ambayo wanakuwa wanayatoa yanaonekana kupindisha sheria za soka kwa makusudi au kwa kutojua sheria.
Suala hilo limekuwa kama sugu na sasa utaona kelele zinaishia mitandaoni tu baada ya hapo vyombo husika ndipo huchukua hatua. Tuliona wakati Pascal Wawa akimkanyaga Ditram Nchimbi live kupitia Azam TV mpaka leo kimya.
Sawa tunakubali mwamuzi hakuona je, zile picha za video hazionyeshi ushahidi? Kama wahusika nao wataendelea kufumbia macho matukio yanayoendelea kujitokeza kwenye ligi basi na waamuzi nao wataendelea kuchukulia poa tu.
Wimbo kuhusu maamuzi ya waamuzi umekuwa mkubwa sasa, promo wanayopewa inatosha nadhani wahusika ambao ni wasimamizi wa ligi yetu wasimamie kuhakikisha kila upande unasimamia haki.
Kuna matukio mbalimbali ambayo yanatokea uwanjani lakini kwa makusudi utakuta baadhi ya waamuzi wakiyafumbia macho pasipo kutoa adhabu yoyote.
Ukiangalia malalamiko ni mengi kwa waamuzi na baadhi ya watu mitaani na hata mitandaoni hudhani pengine wanahusika kupokea kitu kidogo ili kuzibeba timu pinzani.
Shutuma hizo zimekuwa zikistawi kwa muda mrefu na sasa Shirikisho la Soka Tanzania kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi wanatakiwa kuwa macho kwelikweli, tunataka tupate timu shindani kimataifa siyo ya kwenda kusindikiza.
Kama ni kweli kuna waamuzi wanadai chao au hawapewi kwa wakati basi Bodi ya Ligi na TFF hakikisheni hao watu wanalipwa maana kazi wanayofanya ni ngumu na ina vishawishi vingi.
Inasikitisha sana kuona mwamuzi mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘Fifa’ akipindisha sheria, kwa kweli siyo vizuri kila upande usimamie haki.
Kila timu ishinde kwa kile walichostahili kukipata, tusilazimishe ushindi kwa timu fulani maana huo ni uonevu na Mungu hapendi, badilikeni jamani huu ni mwaka 2020.
Timu nyingi zinaishi maisha ya tabu zinasafiri umbali mrefu kwa basi zinafika uwanjani na kujituma kwa nguvu halafu wanatokea watu wanawanyang’anya tonge mdomoni wakati walilifanyia kazi, inasikitisha kwelikweli.
Uchungu wanaoupata hakika siku ya mwisho ninyi mnaowafanyia mabaya lazima nanyi utawarudia. Inaumiza sana.
|
January 27, 2020
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ya yondan kumtemea mate kwas hukuyaona? au Pascal Wawa ndio kafanya ajabu Sana jitahid kuchambua kila tukio sio tuu ya simba bhana ebu balance uwe mchambuz wa soka sio wa Tim fulan
ReplyDeleteni kweli waamuzi wafuate sheria 17 tuone kama Yanga hawatapata kadi nyekundu kila mchezo..
ReplyDeletekuweka picha ya simba na mwadui hapo juu ni upuuzi..kama jana sheria zingefuatwa zote Yanga kulikuwa na kadi nyekundu..
Tatizo lenu mnamihemuko na timu yenu hiyo hamtaki isemwe sawa basis mnunueni naye huyo kama mnavyonunua mechi iliasiweanawandika vibaya aiandike yanga tu
ReplyDelete