January 18, 2020


LUCY Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga leo ameiongoza timu yake kupoteza kwenye mechi yake ya pili kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC, Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa leo ambao ulichezwa huku mvua ikinyesha  kipindi cha kwanza, ulikuwa na  ushindani kwa timu zote ila mwisho wa siku Azam FC wakasepa na pointi zote tatu.

Bao pekee la ushindi la Azam FC lilipatikana kupitia kwa Ally Mtoni 'Sonso' aliyejifunga katika harakati za kuokoa mpira uliopanguliwa na mlinda mlango Faruk Shikalo kutokana na kona iliyopigwa na Bruce Kangwa.

Mchezo wa kwanza kwa Eymael aliyechukua mikoba ya Mwinyi Zahera kufungwa ulikuwa dhidi ya Kagera Sugar ambapo alifungwa mabao 3-0.

Juma Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa walijipanga kupata matokeo mazuri ila bahati haikuwa yao, mashabiki waendelee kuwapa sapoti.

Sure Boy wa Azam FC amesema kuwa wamepata matokeo hayo kutokana na kufuata maelekezo ya mwalimu.

Ushindi huo unaifanya Yanga isalie na pointi 25 ikiwa imecheza mechi 14 huku Azam FC ikijiongezea jumla ya pointi 32 nafasi ya pili.

12 COMMENTS:

  1. Vyuraaaaaaa hawoooooo kambareeeee

    ReplyDelete
  2. GSM ongeza wachezaji wapya jahazi lazama

    ReplyDelete
  3. YANGA hali tete harufu ya kushuka daraja imetanda Jangwani. Inaogepesha kwa kweli kha!

    ReplyDelete
  4. Sasa timu zitanyanganyiana kucheza na Yanga kwakuwa njia nyepesi kujipatia point tatu

    ReplyDelete
  5. Hii ndio faida ya unafiki kwani timu inayojiita ya wananchi ilikejeli sana Simba kuwa chini ya uekezaji lakini cha kushangaza hafla vu wananchi hao wametiwa mfukoni na GSM wanaburuzwa kama ng'ombe aliefungwa kamba ya pua.Badilisha Zahera mwenye akili ya timu kujiendesha sawa.Badilisha Mkwasa kwa sababu Simba ina kocha mzungu sawa. Badilisha nusu kikosi ili Yanga ionekane ina pesa sawa.sasa haya ndio matunda yake. Ila Kwa hekima tu Yanga kubadilisha kocha na wachezaji ishatosha kwani ili timu iwe imara lazima kocha na wachezaji wakae kwa pamoja kwa muda mrefu. Au ikashindikana moja kati ya kocha na wachezaji mmoja wapo wawe wamedumu kwa muda mrefu.Mfano Simba kocha mpya ndio lakini wachezaji wapo pamoja kwa muda mrefu sasa ni rahisi kumrahisishia kazi kocha.Yanga wawe watulivu wampe muda kocha na wasidanganyike kuwa wanaweza kushindana na Simba kwenye mbio za ubingwa wakiandae kikosi hiki hiki kwa ajili ya msimu ujao wa ligi watatisha na watafanikwa sana.Ni ushauri wa bure la sivyo Yanga watapotea wasijue nini wanafanya.

    ReplyDelete
  6. Leo hawawapi wachezaji guard of honor kama ya siku na Kagera?Au Leo wameanza kujua ukweli.

    ReplyDelete
  7. Masikin vyuraaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  8. Saleh Ally eti kuwapa guard of honor wachezaji waliofungwa ndio tatibu wa mpira wetu!!!Ujinga mtupu .Sisi Yanga tuukubali ujinga wa kushangilia kufungwa.

    ReplyDelete
  9. Hofu yangu ni kuwa MASHABIKI WENYE HASIRA WA YANGA MSIANZISHE KAMPENI KUDHURU MAREFA KWANI AMANI ITAONDOKA VIWANJA VYA SOKA. OMBI BODI YA LIGI NA TFF WAAMBIENI WAAMUZI WACHEZESHE KWA HAKI KWANI LA SIVYO UMEWASIKIA MASHABIKI WA YANGA NA MIKAKATI YAO!

    ReplyDelete
  10. sasa isalie na point 25 kwa meche 14 je ipo nafasi ya ngapi

    ReplyDelete
  11. Yanga imeanza kuvuta kasi. Mchezo wa Kwanza na kocha mpya tulipata kichapo cha 3 0 Kutoka kwa timu laiini lakini mechi yapili na Azam tulipsta kichapo cha goli moja sufuri tu, Jee hayo sio maendeleo na mechi ijayo Tunatarajiya droo, Jee hayo pia sio Maendeleo na baada ya hapo tunaanza upya resi ya kunyakuwa ubingwa na kuomba hela tukabidhiwe wenyewe tuamuwe tukitakacho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic