FT :Azam FC 1-0 Yanga
Uwanja wa Taifa
Goli la kujifunga dk 25, Ally Mtoni 'Sonso'
Zinaongezwa dakika nne
Dakika ya 90+3 Kibaya anaingia akichukua nafasi ya Idd Seleman wakati Azam ikipiga kona ambayo haileti matunda Dakika ya 89 Kangwa anachezewa rafu na Ikpe Dakika ya 88 Said Juma anaingia kuchukua nafasi ya Tshishimbi Dakika ya 86 Tshishimbi anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 81 Kocha wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 80 Mtoni anaonyeshwa kadi nyekundu ya mojakwamoja kwa kumchezea faulo Wadada
Dakika ya 78 Ikpe anaingia akichukua nafasi ya Mapinduzi
Dakika ya 77 Chilunda anatoka nje nafasi yake inachukuliwa na Ngoma
Dakika ya 76 Bryson wa Azam FC anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Nchimbi
Dakika ya 73 Juma Abdul anapiga kona mbili zote hazileti matunda
Dakika ya 71 Kaseke anafanya jaribio akiwa nje ya 18 linaleta kona haileti matunda
Dakika ya 69 faulo ya Molinga inapaa kidogo karibu na lango la Abarola
Dakika ya 68 Kaseke anachezewa faulo karibu na eneo la 18
Dakika ya 67 anatoka Chirwa anaingia Nevere
Dakika ya 68 Juma Abdul, Mapinduzi Balama anazuiwa na mabeki wa Azam
Dakika ya 60 Chirwa anachezewa rafu
Dakika ya 56 Ditram Nchimbi anaingia kuchukua nafasi ya Patrick Sibomana
Dakika ya 54 Mahundi anapeleka mashambulizi kwa Shikalo
Dakika ya 50 Chirwa anafanya jaribio halizai matunda
Dakika ya 48 Niyonzima anafanya yake kwa Azam kwa kuwachambua wachezaji kadhaa
Dakika ya 47 Idd anafanya jaribio kwa Shikalo linakwenda nje
Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Taifa
HT:Azam FC 1-0 Yanga
OG: Ally Mtoni dakika ya 25
Zinaongezwa dakika 2
Mpira kwa sasa Uwanja wa Taifa ni kati ya Azam FC dhidi ya Yanga ikiwa ni kipindi cha kwanza.
Mtoni anajifunga bao dakika ya 25 katika harakati za kuokoa mpira uliopanguliwa na mlinda mlango, Farouk Shikalo baada ya kona kupigwa na Bruce Kangwa.
Obrey Chirwa dakika ya 23 alionyeshwa kadi ya njano.
Mpira unachezwa licha ya mvua kunyesha kwa sasa Uwanja wa Taifa.
Anasema Zahera kama hunijui mimi basi jaribu mwengine
ReplyDeleteAibu gani hii jamani yanga yetu mbona hivi eti?mna matatizo gani??
ReplyDeleteTimu ya kwenye vyombo vya habari lakini uwanjani Mh! Hata siku ya mechi ya Simba kadi nyekundu Yanga iliwahusu ila refa alijifanya kubalanzi mchezo. Hata moja ya goli lao ilikuwa faulu ya wazi kabisa. Yanga hamna kitu kama marefa siku zote watazingatia sheria 17 za soka. Yanga hawana nidhamu na wataendelea kuteseka.Backline yao yote haina nidhamu si Dante,si Moro,si mtoni. Huyo Yondani ndio usiseme ila waache waendelee kusheherekea ushindi wa sare zidi ya Simba ila ligi sio kukamia na kuabudu nguvu za giza kwenye mechi ya simba peke yake. Shida zaidi inawasubiri Yanga watakapotoka mikoani.Walibahatisha kwa kibonde chao cha muda mrefu prison na baada hapo kwisha habari.
ReplyDeleteIle droo na Simba walishangilia sana. Walikuwa wanaelezea makosa ya refa waliyonufaika Simba wakasahau uwepo wa Yondani ilikuwa faida kubwa sana kwao maana alistahili kadi nyekundu. Wakati Simba wanahangaikia kutatua tatizo la kupata matokeo kwa timu zinazojaza bingo wakati hawa jamaa wanazidi kuongeza wachezaji wapya kwahio bado sana
Delete*viungo
DeleteThis is yanga brother,timu ya wananchi.inabebwa mpaka aibu hakuna mechi tanga inacheza wakakosa kadi nyekundu ila tu marefa wanawabeba sana,hatimae leo kimejulikana na bado mtaendelea kuteseka sana.
ReplyDeleteHapo mwananchi umechapia ulitaka kusema YANGA sio tanga,pole sana huo ndio mpira wa yanga tunayoijua wala msishangae maana wanavuna walichokipanda ha ha ha ha ha,jaribuni kurudi kwa babu akawatoe hayo manguvu ya giza labda mnaweza mpate ahueni,mmezid kua wachawi wajinga nyinyi angalia sasa unavyowatokea puani,au hamjamlipa babu wa sumbawanga hela zake maana yule wa morogoro ameshazoea kudhulumiwa.
ReplyDelete