UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Ihefu utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.
Ihefu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza itaikaribisha Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho utakaochezwa majira ya saa 10:00 jioni.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa vijana wapo tayari kwa ushindani na wanaamini mechi itakuwa ngumu.
"Vijana wapo tayari na maandalizi yapo sawa ni suala la kusubiri muda uzungumze kwani mpira ni mchezo wa ndani ya uwanja.
"Maandalizi yamekamilika salama na morali ya wachezaji ipo juu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao," amesema.
Azam FC ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho walilitwaa baada ya kushinda fainali mbele ya Lipuli FC kwa ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Obrey Chirwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment