JERRY Muro aliyekuwa Ofisa Habari wa Yanga zamani na sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amesema kuwa anaamini Klabu ya Yanga bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Muro amesema kuwa walikuwa kimya kwa muda mrefu na sasa wameamua kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo yao.
Yanga ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 41 imecheza mechi 22 kinara wa ligi ni Simba mwenye pointi 62 amecheza mechi 24.
"Tumekuwa kimya kwa muda mrefu kwa sasa tunarudi na kazi ya kwanza inaanza kwenye mchezo wetu dhid ya Gwambina baada ya kumalizana na hao hesabu zetu ni kuona tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
"Kila kitu kinawezekana kwani kwa sasa hakutakuwa na sare tena zaidi ya ushindi kutokana na kupata namba za kubonyeza yaani pasword wale ambao wanatubeza watashangaa kuona namna tunavyopenya kwenye mambo wasiyotarajia," amesema.
Kelele za vyura...
ReplyDeletehata wanunue mechi ubingwa labda waibe kombe
ReplyDeleteHawa jamaa wana vituko vingi vya kuchekesha, Huenda mganga kawapa ahadi hiyo baada ya kuchota chake
ReplyDeleteAnasema alikuwa kimya kwa muda mrefu na ili atamke ndio akatamka na Bila ya shaka vyura walimpigia makofi
ReplyDelete