AZAM FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba, mwezi Januari,2020 imeweka rekodi ya kucheza mechi tano bila kupoteza mchezo .
Kwenye mechi tano ilizocheza sawa na dakika 450 haijaruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu huku ikilazimisha sare moja pekee.
Imeshinda jumla ya mechi nne ilizocheza na mwezi Februari ilianza kwa kutoshana nguvu na Mbeya City kwa kufungana bao 1-1, Uwanja wa Samora.
Kesho Jumatano, Februari,5 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons ambayo ilishinda mchezo wake wa kwanza mwezi Februari mbele ya KMC kwa bao 1-0.
Kwani simba kafungwa mechi gani?acha ujinga wewe tena kashinda kwa kishindo kikubwa magoli sio chini ya mawili,tangu januari simba imesuluhu mechi moja tu dhidi ya yanga,zilizobaki zote ameshinda kwa goli zaidi ya mbili.na asipopewa kocha bora mtatueleza mnatumia vigezo gani.
ReplyDeleteMechi moja tu dhid ya lipuli ndio alishinda goli 2 ilichezww tarehe 15.1.2020 zilizobaki zote moja,acheni sifa.
ReplyDelete