ISHU ya ITC ya wachezaji wote waliosajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo msimu huu bado inasubiri maamuzi kutoka FIFA.
Simba ilisajili wachezaji wawili tu ambao ni viungo, Shiza Kichuya aliyekuwa akikikipiga Misri na Luis Miquissone aliyekuwa akikipiga UD do Songo.
Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa wachezaji hao wote bado wanasubiri maamuzi kutoka Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA, ipo hivi:-
Shiza
Kichuya - ITC ilitolewa na Shirikisho la Soka la Misri lakini baadae
ikasitishwa. Kwasasa yanasubiriwa maamuzi ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya
FIFA kuhusu jambo hilo.
Luis Miquissone - ITC bado haijatolewa. Jambo hilo linafanyiwa kazi na FIFA.
Majibu ya mwanzoni FIFA walihitaji maelezo zaidi na tuliwatumia Jumamosi
iliyopita. Kwasasa yanasubiriwa maamuzi ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya FIFA.
Kwa sababu ni wachezaji. Kitu kizuri mara nyingi huwa hakipatikani rahisi.
ReplyDelete