February 9, 2020


ALISSON Becker raia wa Brazil mlinda nyavu za Liverpool amegomea kula bata wakati wa mapumziko na badala yake anaendelea kufanya mazoezi kujiweka fiti.

Mlinda mlango huyo ana jumla ya Clean Sheet 30 tangu aanze kuitumikia timu ya Liverpool.

Wakati huu wa mapumziko anaendelea kupiga tizi na timu ya Fluminense ya Brazil.

Inaelezwa kuwa kila siku anaonekana mazoezini kwenye timu hiyo akiwa na kakaye Muriel ambaye anaidakika timu ya Rio De Janeiro ya Ligi Kuu ya Brazil.

Mastaa wenzake wa Liverpool wengine wamekwenda Dubai kula bata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic