February 11, 2020


Chuo Kikuu cha Jimbo la Colorado eneo la Pueblo nchini Marekani kitaanza kutoa digrii katika masuala ya bangi kuanzia Agosti mwaka huu. Digrii hiyo itaitwa Bangi, Bayolojia & Kemia, na italenga kujifunza sayansi inayohitajika katika kulima na kutengeneza bidhaa za bangi.

Uamuzi huo unafuatia kustawi na kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi nchini humo.

Tangu mwaka 2014, watu wenye umri zaidi ya miaka 21 katika jimbo hilo wameruhusiwa kutumia bangi kama burudani, na kulifanya jimbo hilo kuwa la kwanza nchini humo kutoa ruhusa hiyo.

Hadi kufikia mwaka  2019,  jimbo hilo lilipata zaidi ya dola bilioni moja katika mapato kutokana na biashara hiyo, ambapo fedha hiyo inatumika katika huduma za jamii.

Zaidi ya dola bilioni 6.5 zilitumika katika bidhaa zinazotikana na bangi tangu kuhalalishwa kwake ambapo biashara hiyo imezidi kuimarika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic