February 26, 2020


FT: Yanga 1-0 Gwambina FC
Uwanja wa Uhuru.

Mpira umekamilika Uwanja wa Uhuru kwa Yanga kupenya hatua ya robo fainali.

Kipindi cha pili Gwambina walijitahidi kupambana kutafuta bao na Yanga ilikaza kwa kulinda bao hilo la ushindi

Dakika ya 45+2 Niyonzima Goool

Haruna Niyonzima anafunga bao akiwa nje ya 18 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 

Dakika ya 27 walipata muda wa kupooza koo kidogo

Gwambina wameonekana wakiwa watulivu na kuliandama lango la Yanga.
Timu zote zinacheza mpira wa kushambuliana na kujilinda.

Dakika 15 za mwanzo zimekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu bila timu kufunga.

YANGA leo imeikaribisha Gwambian FC Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mshindi wa leo anapenya jumla mpaka hatua ya robo fainali kuendeleza mbio za kusaka ubingwa uliopo mikononi mwa Azam FC.

Mashabiki wamejitokeza Uwanja wa Uhuru kushuhudia pambano.

4 COMMENTS:

  1. hadi sasa dak 20 na ushee Yanga wanachezewa kama vile wametoka kuhama!jamani Yanga

    ReplyDelete
  2. Yanga anachezewa nusu uwanja..pasi kama simba

    ReplyDelete
  3. Yanga wakicheza na kitimu dhaifu, wametumia kikosi chao cha Kwanza kabisa tena kiwanja cha nyumbani ambapo Simba walitumia karibu 80% wacheziaji wa akiba kupambana na Stand United ya Superl league tena ugenini. Katika mechi zijazo za FA Simba inabidi nao wasidharau wakaipa Yanga kicheko nao watumie kikosi cha kwanza

    ReplyDelete
  4. Kwahakika Yanga walielemewa vibaya na ilikuwa kwa bahati tu kukipata hicho kigoli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic