SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa sasa anatengeneza mfumo mpya utakaompa matokeo chanya kwenye mechi zake anazocheza.
Sven ameshinda mechi sita na kupoteza mechi moja alizosimamia mwezi Februari.
Machi 8 ana kazi ya kumenyana na Yanga, Uwanja wa Taifa alilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza.
Jana aliiongoza Simba kushinda mbele ya Stand United kwa kushinda hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho kwa penalti 3-2 baada ya dakika 90 kutoshana kwa kufungana bao 1-1.
"Bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuna mpango wa kuboresha mfumo mpya wa kikosi chetu ili kupata matokeo kwenye mechi zetu tutakazocheza," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment