Mchezaji wa zamani na aliyewahi kuwa kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo maarufu 'Julio' amesema kuwa klabu ya Simba ilikosea kumuondoa kocha Patrick Aussems wakati timu yake ilikuwa imeshajengeka.
Amesema hayo katika kipindi cha Kipenga Xtra kinachorushwa na East Africa Radio, wakati wa mjadala wa nini kinachoisumbua klabu ya Simba hivi sasa.
Julio amesema kocha yoyote anahitaji kupewa muda wa kutosha katika timu ndipo matunda yataanza kuonekana, akimtolea mfano kocha Aussems kuwa japo alifukuzwa lakini tayari alikuwa na kikosi bora na kilichotulia.
"Simba pale kuna tatizo kwa sababu mpaka tunamfukuza Uchebe tulikuwa tunaongoza ligi, hapo utasemaje?", amesema Julio.
Aidha Julio amefafanua kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa Simba ina wachezaji wazee, ambapo amesema hakumaanisha kuwa hawastahili kucheza lakini kuna mazingira wanashindwa kuendana nayo na kusisitiza kuwa yeye ni mzalendo wa timu hiyo na inamsaidia kwa mambo mengi.
CHANZO: EAST AFRICA TV








Kwani Julio hivi sasa anaikochi timu gani?
ReplyDeleteaache ujinga kwa hiyo huyo uchebe we anaondoka eneo lake la kazi bila ruhusa ya waajili wake haya unaitwa kuja kueleza kwa nn uliondoka unakataa we unategemea mwajili wako achukue hatua gani
ReplyDeleteKocha huyu mpya wa Simba ni bonge la kocha na Aussems kamwe hawezi kuvaa viatu vyake.kocha huyu ameshatwaa klabu bingwa Africa akiwa kocha msaidizi Cameruni. Na licha yakuwa hakudumu kwenye timu ya Taifa ya Zambia lakini kile kitendo cha kuwabwaga makocha kadhaa waliokuwa wakiwania kuifundisha timu hiyo ni dalili tosha kuwa jamaa ni kocha ila watanzania vihere here vimezidi na kujifanya tunajua sana. Kocha katika kauli zake za mwanzo kabisa alisema atahakikisha kumpanga kila mchezaji ili kujua kila uwezo wa mchezaji na katika kipindi hiki ndipo wajuaji wakaanza kumpangia kocha wachezaji wa kuwachezesha. Kocha alipanga fowadi mmoja mbele peke yake si kwamba ilikuwa ni fomesheni bali kwa lengo la kutaka kusoma vizuri uwezo binafsi wa kila fowadi. Licha ya makelele ya watu ila nina hakika kabisa kocha wa Simba kwa mbinu zake hizo tayari sasa ameshakuwa na uweledi wa kutosha kabisa juu ya uwezo wa wachezaji mmoja mmoja na Ukiangalia kikosi cha Simba zidi ya mtibwa utajua kabisa luws benchi la ufundi la Simba tayari limeshapata first eleven matata kabisa .
ReplyDelete